Nenda kwa yaliyomo

Landon Pearson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Landon Pearson


tarehe ya kuzaliwa (1930-11-16)16 Novemba 1930
Toronto, Ontario, Canada
tarehe ya kufa 28 Januari 2023 (umri 92)
Ottawa, Ontario, Canada
chama Liberal
ndoa Geoffrey Pearson (m. 19512008) «start: (1951)end+1: (2009)»"Marriage: Geoffrey Pearson to Landon Pearson" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Landon_Pearson)
watoto 5 (akiwemo Patricia Pearson)
mhitimu wa Trinity College, Toronto
University of Ottawa
Fani yake
  • Uandishi
  • Mtetezi wa Haki za Watoto

Landon Carter "Lucy" Pearson (alizaliwa tarehe 16 Novemba 1930, na alifariki 28 Januari 2023) alikuwa Seneta wa Kanada na mtetezi wa haki za watoto. Alikuwa binti mkwe wa Waziri Mkuu wa zamani Lester B. Pearson, kupitia ndoa yake na mwanawe Geoffrey Pearson.

Pearson aliteuliwa kuwa Seneta wa Kanada mnamo tarehe 15 Septemba mwaka 1994 na Waziri Mkuu wa wakati huo Jean Chrétien na akaketi katika kikao cha Liberal. Alistaafu kutoka Seneti mnamo Novemba 16 mwaka 2005 alipofikisha umri wa kustaafu wa lazima wa miaka 75.

Kama Mwandishi

[hariri | hariri chanzo]

Kitabu chake cha, "Children of Glasnost (1990)"[1] kilielezea yeye kukulia katika umoja wa kisovieti na jinsi ilivyobadilisha jamii ya kirusi na kuwa wazi zaidi. Kitabu chake cha pili, "Letters from Moscow", uchaguzi wa mwitikio binafsi alipokuwa akiishi jijini Moscow wakati mume wake alipokuwa balozi wa Kanada nchini Urusi (Umoja wa Kisovieti) kilichapishwa mwaka 2003. Mnamo mwaka 2010 kwa kushirikiana na Daktari wa Philosofia Judy Finlay (PhD), Pearson alichapisha Tibacimowin: Mkusanyiko wa simulizi zilizokusanywa na kutafsiri simulizi za kihistoria kutoka kwa wanachama wa Taifa la kwanza la wazee wa Ontario.

  1. "Children of Glasnost: Growing Up in Soviet". Publishers Weekly. 4 March 1991. Landon Pearson, Author University of Washington Press ISBN 978-0-295-97090-5
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Landon Pearson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.