Kwinini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
 Magome ya mti wa Cinchona officinalis
Magome ya mti wa Cinchona officinalis

Kwinini ni alkaloidi ambayo inaweza kupunguza homa, inayofanya kazi dhidi ya malaria, maumivu na uvimbe. Gome la mti wa familia ya Cinchona imejaliwa kwinini ya asili. Mti huo unapatikana huko Andes, Amerika ya Kusini, Indonesia, na Kongo.

Kwinini inaweza pia kutengenezwa na binadamu, lakini hii ni ghali zaidi, hivyo ni bora kuichukua kutoka kwenye magome ya miti.

Kwinini ilikuwa tiba ya kwanza ya malaria, iliyojulikana huko Ulaya mwaka 1631, na labda mapema kwa watu wa asili wa Amerika ya Kusini.

Hata leo, kwinini hutumiwa kutibu aina fulani za malaria, wakati dawa nyingine zinashindwa au hazipatikani. Kwa njia hiyo, kwinini kwa sasa ni mojawapo ya tiba bora zaidi ya malaria, ambayo husababishwa na plasmodiamu aina ya falciparum. Kwa aina nyingine za malaria, kwinini haitumiki tena.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kwinini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.