Kwaya ya Wasichana ya Cantamus
Kwaya ya Wasichana ya Cantamus ni kwaya yenye makao katika Mansfield, Nottinghamshire na lina takriban wasichana arobaini wenye umri kati ya miaka kumi na tatu na kumi na tisa. Kwaya hii ilianzishwa mwaka wa 1968 na Pamela Cook (Mkurugenzi), Geoffrey Thompson (mumewe Cook na Mweka hazina), Sheila Haslam (Katibu) na Ivan Haslam (mwuuzaji wa Tiketi na CD). [1] Archived 12 Machi 2007 at the Wayback Machine.
Michael Neaum akawa kiongozi mwaka wa 1976. Ann Irons alijiunga kama Mkurugenzi Msaidizi mwaka wa 1976. Elaine Guy alikuwa mwanachama wa zamani na akawa mkufunzi wa sauti mwaka 1983. Joy Nicol akawa mwalimu wa sauti mwaka wa 1995. Philip Robinson aliteuliwa kama kiongozi mwaka wa 200 [2] Archived 12 Machi 2007 at the Wayback Machine.
Mataji mashuhuri ambayo kwaya hii imeshinda ni taji la kwaya ya Dunia mwaka wa 1997 katika Llangollen Eisteddfod, taji la mabingwa wa Olimpiki katika Michezo ya kwaya ya Dunia mwaka wa 2004 na 2006 na tuzo la Grand Prix katika tamasha ya Riva de Garda mwaka wa 1996.
Hivi karibuni Cantamus ilishiriki katika michezo ya nne ya kwaya ya Dunia huko Xiamen, China mwezi Julai mwaka wa 2006, na kushinda medali mbili za dhahabu, na kufanikiwa kupata alama ya juu zaidi katika shindano hili na alama ya 89.13
Kwaya ya Cantamus waliimba katika tamsha yao ya kwanza kwa umma mwaka wa 1968 na tangu wakati huo wasichana 340 wameimba pamoja na Cantamus.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 1971 - Shindano la Kimataifa la kuimba la Montreux-Nafasi ya pili
- 1972 - Tamasha ya muziki wa aina ya Contemporary ya Bela Bartok , Debrecen, Hungaria - Nafasi ya kwanza
- 1972 - BBC Radio 3 "Let the People Sing" - Washindi wa raundi ya Uingereza
- 1978 - Shindano la Kimataifa la kuimba la Montreux- Nafasi ya kwanza mara mbili (Majaji na watazamaji)
- 1979 - Tamasha ya kimataifa ua kuimba ya Międzyzdroje, Poland - Nafasi ya kwanza
- 1980 - Llangollen Eisteddfod - Nafasi ya kwanza(Daraja la vijana)
- 1982 - Tamasha ya muziki na vijana ya Vienna - Nafasi ya kwanza (Daraja ya kwaya za kina dada)
- 1982 - Tuzo la Mji mkuu wa Vienna kwa kuwa kwaya bora zaidi katika tamasha
- 1986 - Tamasha ya kimataifa ya kuimba ya Montreux- Nafasi ya kwanza (watazamaji)
- 1986 - Shindano la BBC / Sainsbury la "kwaya wa Mwaka" - Nafasi ya kwanza (Sahemu ya watu wazima)
- 1986-1990 - Tuzo la Performing Rights Society kila mwaka kwa ajili ya biashara
- 1994 - la BBC / Sainsbury la "kwaya wa Mwaka"- Nafasi ya kwanza (sehemu ya vijana)
- 1995 - Tamasha ya kimataifa ya kuimaba, Tolosa, Uhispania - Nafasi ya kwanza (kwaya ya kina dada)
- 1996 - Shindano la kimataifa la kuimba la Riva del Garda- Grand Prix
- 1997 - Llangollen International Eisteddfod - Kwaya ya Dunia
- 1998 - Tamsha ya muziki ya vijana ya Ulaya, Neerpelt, Ubelgiji - Summa cum Laude (Kwaya Kuu na Kwaya ya Mafunzo)
- 2002 - Tamasha ya kuimba ya kimataifa ya Arezzo: Nafasi ya kwanza (daraja ya nyimbo za kitamduni); Nafasi ya tatu (daraja ya Polyphony); Nafasi ya tatu (daraja ya Plainchant)
- 2004 - Olimpiki ya kwaya ya dunia, Bremen, Ujerumani: medali mbili za dhahabu (madaraja ya sauti sawa na nyimbo ya kitamaduni zinazoandanwa ); Taji la mabingwa wa Olimpiki
- 2006 - Olimpiki ya kwaya ya dunia, Xiamen, Uchina: Medali mbili za dhahabu(madaraja ya sauti sawa na nyimbo ya kitamaduni zinazoandanwa ); Kwaya yeny alama nyingi katika shindano hili; Taji la mabingwa wa Olimpiki
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- 2001 - Cantamusaurora - Warner Music 8573-87312-2
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- tovuti rasmi Archived 15 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
- Jukwaa rasmi ya Cantamus Archived 14 Mei 2009 at the Wayback Machine.