Kasoko ya dharuba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kreta ya dharuba)
Kutokea kwa kasoko ya dharuba
Kutokea kwa kasoko kutokana na dharuba (filamu ya maabara ya NASA)

Kasoko ya dharuba (kwa Kiingereza impact crater) ni uwazi kwenye ardhi unaotokana na mshtuko wa kugongwa na gimba. Kasoko ina umbo la duara; katikati ni kama shimo na ukingo wake unainuka juu ya uwiano wa mazingira yake. Duniani kasoko zinapatikana mara nyingi kutokana na milipuko ya volkeno au milipuko mingine.

Katika magimba ya angani yenye uso thabiti kuna kasoko nyingi kama matokeo ya kugongwa na magimba kutoka anga-nje. Kwa mfano, kwenye Mwezi wa Dunia kuna kasoko nyingi zilizosababishwa na migongano ya asteroidi au vimondo. Pigo la kitu kigumu linarusha mata iliyopo mahali pa mgongano ikae pembeni kwa shimo hilo kwa umbo la ukingo wa mviringo.

Duniani kasoko nyingi kutokana na mishtuko ya aina hiyo zinasawazishwa baada ya muda fulani kutokana na mmomonyoko unaosababishwa na mvua na upepo; kwenye magimba pasipo angahewa kama Mwezini zinabaki kwa miaka milioni kadhaa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kasoko ya dharuba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.