Nenda kwa yaliyomo

Konstantinos Tsimikas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tsimikas akiichezea Liverpool mwaka 2022

Konstantinos Tsimikas (alizaliwa 12 Mei 1996) ni mchezaji wa soka wa Ugiriki ambaye anacheza kama beki wa kushoto katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool na timu ya taifa ya Ugiriki.[1][2]

Tsimikas hapo awali alichezea timu ya mpira ya Olympiacos, na pia alikuwa kama mchezaji wa mkopo katika timu ya mpira ya Esbjerg na Willem II.

Maisha katika klabu

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni

[hariri | hariri chanzo]

Tsimikas alizaliwa huko Thessaloniki, na anatokea katika kijiji cha Lefkonas, Serres.[3]Alianza kucheza mpira katika timu ya kijijini kwake na akahamia AS Neapoli Thessaloniki alipokuwa na umri wa miaka 14. Mnamo 2013, alihamia Panserraikos na alifunga mabao 5 msimu wa 2013-14 huko Gamma Ethniki.[4]

Olympiacos

[hariri | hariri chanzo]

Tsimikas alicheza mechi yake ya kwanza Olympiacos katika kombe la Super League katika mechi dhidi ya AEL Kalloni tarehe 19 Desemba 2015.

Mkopo hadi Esbjerg

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 28 Desemba 2016, Tsimikas alisaini mkataba na klabu ya Esbjerg ya Denmark kwa mkopo, hadi mwisho wa msimu wa 2016-17.Mnamo tarehe 17 Februari 2017, katika mechi yake ya kwanza na klabu hio, alifunga bao katika mchezo wa ushindi wa 3-0 dhidi ya SønderjyskE Fodbold. Aliiacha klabu hiyo baada ya michezo 13, na kurudi Olympiacos.

Mkopo hadi Willem II

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 30 Juni 2017, Tsimikas alifanya uhamisho mwingine wa mkopo, wakati huu kwenda kwa klabu ya Uholanzi Willem II kwa mkataba wa msimu mzima.[5] Alikuwa mchezaji wa kawaida kama wachezaji wengine katika ligi ya Eredivisie ya 2017-18, akianza mechi 32 kati ya 34,[6] na pia alifunga mabao 5. Katika robo-fainali ya Kombe la KNVB, mpira wa adhabu ulimpiga na kuingia golini na kusababisha sare ya kuelekea dakika nyingine za nyongeza, na Willem II alipata ushindi katika mikwaju ya penati.[7] Mpira wa tikitaka alioupiga Tsimikas nakupelekea ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya FC Utrecht ulichaguliwa kuwa bao bora la Mwezi Voetbal International na kuchangia kuwa rookie bora wa ligi ya Eredivisie kwa Mwezi Machi 2018.[8]

  1. "Konstantinos Tsimikas". Soccerway. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Konstantinos Tsimikas - UEFA". Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ο Σάκης Αναστασιάδης μιλά για τον "Σερραίο" Τσιμίκα: "Στην πρώτη προπόνηση δεν ακούμπησε μπάλα!"". LiverpoolFans.gr (kwa Kigiriki). 2020-08-12. Iliwekwa mnamo 2021-02-04.
  4. "talentabout.gr Ο ταλαντούχος Κώστας Τσιμικας". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-12. Iliwekwa mnamo 2023-03-15.
  5. "Willem II haalt linksback Konstantinos Tsimikas uit Griekenland", 30 June 2017. (nl) 
  6. "K. Tsimikas". Soccerway. Perform Group. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Burns, Will (2 Februari 2018). "KNVB Beker report: Quarter-finals". Total Dutch Football. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Slip in Tilburg". FC Utrecht. 31 Machi 2018. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
    "Fenomenale goal Tsimikas verkozen tot Doelpunt van de Maand maart" [Tsimikas' phenomenal goal chosen as Goal of the Month for March]. VI.nl (kwa Kiholanzi). 13 Aprili 2018. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
    "Santiago Arias named Player of the Month". Eredivisie. 4 Aprili 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-06. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2019. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Konstantinos Tsimikas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.