Nenda kwa yaliyomo

Konstantino wa Britania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Konstantino wa Cornwall)

Konstantino wa Britania (Dumnonia, Uingereza, 520 hivi - Kintyre, Uskoti, 9 Mei 576) alikuwa mfalme mkatili na mzinzi wa Cornwall[1] kuanzia mwaka 537.

Kisha kuongokea Ukristo, aliacha utawala akawa mmonaki nchini Ireland. Miaka saba baadaye alipewa upadirisho akatumwa kuinjilisha Uskoti chini ya Kolumba. Huko alianzisha monasteri ya Govon aliyoiongoza kama abati hadi alipouawa na Wapagani[2].

Tangu kale anaadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa tarehe 11 Machi[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.