Konrad Krajewski
Mandhari
Konrad Krajewski (alizaliwa 25 Novemba 1963) ni kardinali wa Polandi wa Kanisa Katoliki ambaye anahudumu kama Mkuu wa Kwanza wa Idara ya Huduma za Upendo.
Krajewski alihudumu kama msimamizi wa ibada za kipapa kutoka 1998 hadi 2013. Mnamo 2013, aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Sadaka za Kipapa akisimamia shughuli za misaada za Papa Fransisko kupitia Ofisi ya Sadaka za Kipapa, ambayo ilipandishwa hadhi kuwa Idara ya Huduma za Upendo kwa mujibu wa katiba ya kitume Praedicate Evangelium mnamo Juni 2022.
Papa Fransisko alimteua kuwa kardinali tarehe 28 Juni 2018.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nomina dell'elemosiniere di Sua Santità" (in it). Bollettino (Holy See). 3 August 2013. https://press.vatican.va/content/salastampa/it/bollettino/pubblico/2013/08/03/0513/01145.html. Retrieved 28 November 2017.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |