Nenda kwa yaliyomo

Kombe la Shirikisho la FIFA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kombe la Shirikisho la FIFA (Kiingereza: FIFA Confederations Cup) yalikua ni mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu kwa timu za taifa za wanaume, yaliyokuwa yakifanyika kila baada ya miaka minne chini ya usimamizi wa FIFA. Mashindano haya yalishirikisha kila bingwa wa shirikisho la mpira wa miguu katika mabara yote sita (AFC, CAF, CONCACAF, CONMEBOL, OFC, na UEFA), pamoja na mshindi wa Kombe la Dunia na nchi mwenyeji wa mashindano, hivyo kufanya jumla ya timu nane.

Kati ya 2001 hadi 2017 (isipokuwa 2003), mashindano haya yalifanyika katika nchi ambayo ingetumika kama mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka uliofuata, yakiwa kama jaribio la maandalizi ya mashindano makubwa yajayo.

Mabingwa wa mara ya mwisho walikuwa Ujerumani, waliotwaa wa Kombe la Shirikisho la FIFA mnamo 2017 baada ya kuifunga Chile bao 1–0 katika mchezo wa fainali na hivyo kushinda taji lao la kwanza.

Mnamo Machi 2019, FIFA ilithibitisha kuwa mashindano haya hayataendelea kufanyika tena. Nafasi yake ilichukuliwa na mashindano ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA, pamoja na kuanzishwa kwa mashindano ya 2021 FIFA Arab Cup kama maandalizi ya Kombe la Dunia la FIFA 2022.[1][2]

  1. "FIFA Council votes for the introduction of a revamped FIFA Club World Cup". inside.fifa.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-18.
  2. "FIFA President confirms 22 national teams will participate in FIFA Arab Cup 2021 in Qatar". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kombe la Shirikisho la FIFA kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.