Nenda kwa yaliyomo

Kombe la Dunia la FIFA 2014

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kombe la Dunia la FIFA 2014
Nembo ya Kombe la Dunia 2014
MwenyejiBrazili
Tarehe12 Juni – 13 Julai 2014
Idadi ya timu32
MshindiUjerumani
Mshindi wa piliArgentina
Mshindi wa tatuUholanzi
Kutangazwa kwa Brazili kama mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia ya 2014 mnamo 2007

Kombe la Dunia la FIFA 2014 ilikuwa ni mashindano ya 20 ya Kombe la Dunia la FIFA, michuano inayofanyika kila baada ya miaka minne kwa timu za taifa za wanaume. Mashindano hayo yalifanyika nchini Brazili kuanzia 12 Juni hadi 13 Julai 2014, baada ya nchi hiyo kupewa haki ya kuwa mwenyeji wa mashindano mnamo 2007. Hii ilikuwa mara ya pili kwa Brazili kuandaa mashindano hayo, mara ya kwanza ikiwa 1950, na mara ya tano kufanyika katika bara la Amerika Kusini.

Timu 31 za taifa zilifuzu kupitia hatua za mchujo kujiunga na nchi mwenyeji katika mashindano (ikiwa Bosnia na Herzegovina ndiyo timu pekee iliyoshiriki kwa mara ya kwanza). Jumla ya mechi 64 zilichezwa katika viwanja 12 vilivyoko kwenye miji 12 tofauti nchini Brazili. Kwa mara ya kwanza katika historia ya fainali za Kombe la Dunia, waamuzi walitumia teknolojia ya mstari wa goli (goal-line technology) pamoja na sprei maalum ya kufutika (vanishing spray) inayotumika kuweka alama kwa mipira ya adhabu ndogo (free kicks).[1]

Tamasha la mashabiki wa FIFA katika mji wa Brasília

Tamasha la mashabiki wa FIFA (FIFA Fan Fests) katika kila mji mwenyeji lilivutia jumla ya watu milioni 5, na nchi hiyo ilipokea wageni milioni 1 kutoka nchi 202. Hispania, waliokuwa mabingwa watetezi, walitolewa katika hatua ya makundi. Nchi mwenyeji Brazili, ambayo ilikuwa imeshinda Kombe la Shirikisho la FIFA mnamo 2013, ilifungwa na Ujerumani mabao 7–1 katika nusu fainali na hatimaye kumaliza katika nafasi ya nne.[2]

Katika mchezo wa fainali, Ujerumani iliifunga Argentina bao 1–0 baada ya dakika za nyongeza, kufuatia goli la shuti lililofungwa na Mario Götze katika dakika ya 113 ya mchezo, na hivyo kushinda kombe hilo na kujihakikishia taji la dunia kwa mara ya nne.[3] Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kushinda tangu kuungana kwake mnamo 1990, mwaka ambao (ikiwa kama Ujerumani Magharibi) pia ilishinda dhidi ya Argentina kwa matokeo yale yale ya 1–0 ndani ya dakika 90 katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 1990. Ushindi huo ulikuwa ni wa kwanza kwa Ujerumani katika mashindano makubwa tangu mashindano ya UEFA ya Mataifa ya Ulaya mnamo 1996. Hivyo Ujerumani ikawa timu ya kwanza ya Ulaya kushinda Kombe la Dunia lililofanyika katika Bara la Amerika.[4] Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa hii ilikuwa mara ya tatu mfululizo kwa timu kutoka Ulaya kushinda taji la dunia, baada ya Italia mnamo 2006 na Hispania mwaka 2010, rekodi ya kipekee iliyodumishwa na Ufaransa miaka minne baadae.[5][6]

Timu zilizoshiriki

Baada ya mechi za kufuzu zilizochezwa kati ya Juni 2011 na Novemba 2013, timu 32 zilifuzu kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia 2014.[7] Kati ya timu hizo, ishirini na nne zilikuwa zimerudi kushiriki baada ya kuwa sehemu ya Kombe la Dunia la FIFA 2010. Bosnia na Herzegovina ndiyo timu pekee iliyokuwa ikishiriki kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya Kombe la Dunia.[8]

Kolombia ilifuzu baada ya kukosa mashindano hayo kwa miaka 16, huku Ubelgiji na Urusi zikirudi baada ya kukosekana kwa miaka 12. Paraguay haikufanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994. Aidha, hili lilikuwa Kombe la Dunia la kwanza katika kipindi cha miaka 32 bila kuwa na mwakilishi yeyote kutoka nchi za Kaskazini mwa Ulaya (Nordic countries). Iran, Costa Rica, Ecuador, na Croatia zilirudi kushiriki baada ya kukosa nafasi mwaka 2010. Timu iliyokuwa na nafasi ya juu zaidi katika viwango vya FIFA lakini haikufuzu ilikuwa Ukraini (iliyokuwa nafasi ya 16), ilhali timu iliyokuwa na nafasi ya chini zaidi iliyo fanikiwa kufuzu ilikuwa Australia (iliyokuwa nafasi ya 62).[7]

Waamuzi (Marefa)

Mnamo Machi 2013, FIFA ilichapisha orodha ya waamuzi 52 waliotakiwa kushiriki katika maamuzi ya mshindano, ambapo kila mmoja aliunganishwa na wamuuzi wasaidizi wawili kulingana na uraia wao, kutoka katika mashirikisho yote sita ya mpira wa miguu duniani.[9][10]

Yuichi Nishimura kutoka shirikisho la mpira wa miguu nchini Japani alikuwa mwamuzi wa mechi ya ufunguzi, na Nicola Rizzoli kutoka shirikisho la mpira wa miguu nchini Italia alikuwa mwamuzi wa mechi ya fainali.[11][12]

Makundi

Timu 32 zilizoshiriki ziligawanywa katika makundi manane.

Kundi A Kundi B Kundi C Kundi D
Bendera ya Brazil Brazil Bendera ya Hispania Hispania Bendera ya Kolombia Kolombia Bendera ya Uruguay Uruguay
Bendera ya Kroatia Kroatia Bendera ya Uholanzi Uholanzi Bendera ya Ugiriki Greece Bendera ya Costa Rica Kosta Rika
Bendera ya Mexiko Meksiko Bendera ya Chile Chile Bendera ya Côte d'Ivoire Côte d'Ivoire Bendera ya Uingereza Uingereza
Bendera ya Kamerun Kamerun Bendera ya Australia Australia Bendera ya Japani Japan Bendera ya Italia Italia
Kundi E Kundi F Kundi G Kundi H
Bendera ya Uswisi Uswisi Bendera ya Argentina Argentina Bendera ya Ujerumani Ujerumani Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji
Bendera ya Jamhuri ya Dominika Jamhuri ya Dominika Bendera ya Bosnia na Herzegovina Bosnia na Herzegovina Bendera ya Ureno Ureno Bendera ya Aljeria Aljeria
Bendera ya Ufaransa Ufaransa Bendera ya Uajemi Iran Bendera ya Ghana Ghana Bendera ya Urusi Urusi
Bendera ya Honduras Honduras Bendera ya Nigeria Nigeria Bendera ya Marekani Marekani Bendera ya South Korea Korea Kusini

Viwanja

Viwanja 12 (saba vipya na vitano vilivyokarabatiwa) katika miji 12 vilichaguliwa kwa ajili ya mashindano hayo. Viwanja hivyo vilihusisha maeneo yote ya miji mikubwa nchini Brazili kwa uwiano bora zaidi wa uenyeji ikilinganishwa na mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 1950 yaliyofanyika nchini humo.[13]

Rio de Janeiro Brasília São Paulo Fortaleza
Uwanja wa michezo wa Maracanã Uwanja wa Taifa Mané Garrincha Uwanja wa michezo wa Corinthians
(Uwanja wa michezo wa São Paulo)
Uwanja wa michezo wa Castelão
Uwezo: 78,838[14] Uwezo: 72,788[14] Uwezo: 63,321[14] Uwezo: 60,348[14]
Belo Horizonte


Salvador
Uwanja wa michezo wa Mineirão Uwanja wa michezo wa Fonte Nova
Uwezo: 62,160[14] Uwezo: 51,708[14]
Porto Alegre Recife
Uwanja wa michezo wa Beira-Rio Uwanja wa michezo wa Pernambuco
Uwezo: 51,000[14] Uwezo: 45,440[14]
Cuiabá Manaus Natal Curitiba
Uwanja wa michezo wa Pantanal Uwanja wa michezo wa Amazônia Uwanja wa michezo wa Dunas Uwanja wa michezo wa Baixada
Uwezo: 42,788[14] Uwezo: 44,300[14] Uwezo: 42,000[14] Uwezo: 42,000[14]


Marejeo

  1. "FIFA launch GLT tender for Brazil 2013/14". FIFA.com. 19 Februari 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Passarinho, Nathalia; Matoso, Filipe (14 Julai 2014). "Em balanço da Copa, Dilma diz que Brasil derrotou prognósticos 'terríveis'". G1 (kwa Kireno). Grupo Globo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Juni 2017. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Taylor, Daniel (13 Julai 2014). "Germany beat Argentina to win World Cup final with late Mario Götze goal". The Guardian. Iliwekwa mnamo 1 Septemba 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "If the World Cup started tomorrow". ESPN FC. 12 Juni 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Desemba 2013. Iliwekwa mnamo 4 Desemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Owen, David (14 Julai 2014). "Battle of the Brands: Adidas lifts the World Cup, but Nike scores most goals". Inside World Football. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Numbers Game: All the stats from Germany's fourth World Cup triumph". Firstpost. 14 Julai 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 1 2 3 FIFA.com. "The FIFA/Coca-Cola World Ranking - Ranking Table - FIFA.com". FIFA.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-10-14.
  8. FIFA.com (2014-06-10), "1 day to go", FIFA.com (kwa Kiingereza (Uingereza)), iliwekwa mnamo 2025-10-14
  9. "Referee trios and support duos appointed for 2014 FIFA World Cup". FIFA.com. 15 Januari 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Referees & assistant referees for the 2014 FIFA World Cup" (PDF). FIFA.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 28 Mei 2014. Iliwekwa mnamo 2 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Referee designations for matches 1–4" (PDF). fifa.com. 10 Juni 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 30 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 19 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "2014 FIFA World Cup - Matches". FIFA.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Host cities in 1950 FIFA World Cup". Colunas.globoesporte.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Agosti 2011. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 "2014 FIFA World Cup Brazil Venues". FIFA.com. 18 Januari 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Mei 2019. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)