Klexikon

Klexikon ni ensaiklopidia (kamusi elezo) ya Kijerumani iliyopo na kutumika mtandaoni kwa ajili ya watoto wenye umri wa kati ya miaka sita hadi kumi na mbili. Ilizinduliwa mnamo Desemba 2014. Neno Klexikon ni mjumuisho wa maneno mawili ya kijerumani Kinder (watoto0 na Lexikon (ensaiklopidia). Kama jinsi ilivyo Wikipedia, tovuti hii iliundwa kama wiki kwa kutumia programu ya MediaWiki . Maudhui ya maandishi yanapatikana chini ya leseni ya Creative Commons By Attribution Share-alike toleo la 3.0 huku midia yake ikichukuliwa kutoka Wikimedia Commons . [1] [2] Sheria maalum zilitekelezwa ili kuhakikisha kuwa maudhui yote yanafaa kwa watoto. [3] Zaidi ya hayo, wahariri wote wanatakiwa kujiandikisha kupitia barua pepe. [4]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kamusi elezo ya Klexikon ilianzishwa na mwanahabari Michael Schulte na mwanahistoria Ziko van Dijk, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Wikimedia Uholanzi kuanzia mwaka 2011 hadi 2014. [5] Tovuti hii inamilikiwa na shirika lisilo la faida la Zentrale für Unterrichtsmedien im Internet [online educational media center] ambayo pia huandaa aina tofauti tofauti za Wiki.
Mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa, Klexikon ilikuwa na nakala 1,000 na nakala 1,500 ziliundwa baada ya miaka miwili.[6][7] Jumuiya ya wahariri wa Klexikon huamua kwa makubaliano ni makala gani inapaswa kuundwa ama kuchapishwa ili kuhakikisha kuwa maudhui yenye umuhimu, masomo ya shule na maeneo yanayowavutia watoto yanapewa kupaumbele.[8]
Klexikon ilikuwa ikiendeshwa kwa msaada wa Wikimedia Deutschland kwenye uratibu wa maudhui kwaajili ya watoto.[9] Wazo hilo ambalo lilikuja kuungwa mkono zaidi na Chuo Cha Ufundi Cha Dortmund na Chuo Cha Cologne.[10][11]
Mapokezi
[hariri | hariri chanzo]Wizara ya Ujerumani inayohusika na masuala ya Familia, Raia, Wazee, Wanawake na Vijana imekuwa mbele kutoa umuhimu wa tovuti hii kwa watoto. [12] Kulingana na chama kimoja cha televisheni cha nchini Ujerumani kijulikanacho kama Voluntary Self Control Association of German Television, kilisema kuwa tovuti hii ya Klexikon ina umuhimu mkubwa sana ukilinganisha na Wikipedia ya kawaida kwasababu hii ni mahususi kwa ajili ya watoto.
[13] Tovuti ya Shule ya Austria iliandika kwamba Klexikon ilikuwa "sehemu kubwa ya marejeleo" ambayo ilitoa maudhui ambayo yalitumiwa haswa kwa watoto.[14] Jarida la Merz lilibainisha kuwa Klexikon ilikuwa chanzo kizuri cha habari mtandaoni chenye maudhui ya kutegemewa, lakini lilikosoa kuwa baadhi ya makala hayakutoa vyanzo vyovyote. Hii ilikuwa kinyume na hitaji la kuhamasisha upatikanaji wa maudhui kwaajili ya wanafunzi wa shule za sekondari.[15]
Tuzo na teuzi
[hariri | hariri chanzo]- 2015: Pädi – der pädagogische Interaktiv-Preis (Tuzo za Pedagogical Interactive)[16]
- 2016: Ilichaguliwa kuwania tuzo ya 2016 ya Rasilimali za elimu huria katika kitengo cha "elimu"[17]
- 2017: Tuzo za OER katika kitengo cha "Elimu za mashuleni" [18]
- 2018: "Uvumbuzi kwa Ujerumani" kwenye shindano la mawazo yenye tija [19]
- Seitenstark Seal of Approval for Digital Children's Media, iliyotolewa na Seitenstark e. V. na Wizara ya Shirikisho ya Masuala ya Familia, Wazee, Wanawake na Vijana[20]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "In English". Klexikon. 5 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Freies Wissen". Klexikon (kwa German). 1 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Grundregeln". Klexikon (kwa German). 22 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Grundregeln". Klexikon (kwa German). 22 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Klexikon.de - Wikipedia für Kinder". GEOlino (kwa German). Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Schoener, Johanna (14 Desemba 2015). "Wikipedia für Kinder: Wo bleibt der Pups?". Die Zeit (kwa German).
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Daten zum Klexikon". Klexikon (kwa German). 19 Agosti 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Artikelwünsche". Klexikon (kwa German). 12 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Erhart, Ed (15 Julai 2015). "The Klexikon: a new wiki encyclopedia for children". Wikimedia BLog. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "klexikon.de: Auf dem Weg zu einer Wikipedia für Kinder – Möglichkeiten für den Deutschunterricht" (PDF) (kwa German). Technical University of Dortmund. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Dickmann, Mirka. Schilly, Ute Barbara (mhr.). "Projekt 'Klexikon'" (kwa German). Technical University of Cologne. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Gutes Aufwachen mit Medien. Ein Netz für Kinder" (PDF) (kwa German). Federal Ministry of Family Affairs, Senior Citizens, Women and Youth. uk. 9.
{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "Klexikon.de: Wenn Wissen mitmachen lässt" (kwa German). Freiwillige Selbstkontrolle Fernsehen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-05-18. Iliwekwa mnamo 2017-09-16.
{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Mayrhofer, Sabrina (15 Juni 2016). "Wikipedia für Kinder" (kwa German). Österreichisches Schulportal. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Fleischmann, Katrin (2015). "Klexikon: Eine Wikipedia für Kinder". Merz – Medien + Erziehung (kwa German). Na. 4.
{{cite magazine}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "PÄDI – der Pädagogische Interaktiv-Preis 2015" (PDF) (kwa German). SIN - Studio im Netz e.V. uk. 2.
{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "OER-Award 2016 – Wettbewerb und oer.academy". OERinfo – open-educational-resources.de (kwa German). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 16 Septemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ "OER-Award - OERinfo – Informationsstelle OER", OERinfo – Informationsstelle OER, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-25, iliwekwa mnamo 2017-12-11
- ↑ "Ausgezeichnete Orte im Land der Ideen", Land der Ideen, iliwekwa mnamo 2018-06-26
- ↑ "Neues SEITENSTARK-GÜTESIEGEL - 31 herausragende Kinderwebseiten ausgezeichnet", klicksafe, 2022-12-06, iliwekwa mnamo 2022-12-11
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
media kuhusu Klexikon pa Wikimedia Commons- Main page in Klexikon
| Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Klexikon kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |