Klaus Barbie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Klaus Barbie akivaa sare za SS wakati wa vita.

Klaus Barbie (25 Oktoba 191325 Septemba 1991) alikuwa mwanajeshi wa SS au Schutzstaffel-Hauptsturmführer, na pia alikuwa mmoja wa wanachama wa Gestapo. Alikuwa akifahamika kama the Butcher of Lyon au Mchinjaji wa Lyon.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Klaus Barbie alizaliwa mjini Bad Godesberg, karibu na mji wa Bonn, Ujerumani. Barbie alizaliwa katika familia ya waumini wa dhebu la Wakatoliki. Wazazi wake wote walikuwwa walimu. Kunako mwaka wa 1923 alipelekwa shule ambayo babake ndiko alikokuwa akifundishia. Baada ya hapo, akapelekwa shule ya bweni ya mjini Trier.

Mnamo mwaka 1925, familia yake ilihamia mjini Trier ambako huko ndiko alikokuwa anasoma. Mnamo mwaka wa 1933, babake na kakake kipenzi Barbie waliiaga dunia. Kifo cha babake kilipeleka bwana mdogo Barbie kuwa mlevi kupindukia na ndipo alipo amua kujiunga na jeshi la vijana la Adolf Hitler, waliliita Hitler Youth.

Mnamo Septemba 1935, alijunga na SD au Sicherheitsdienst (kikosi cha ulinzi), ni tawi maalum la SS. Baadae kidogo alihamishwa kwenda kutumikia nchini Uholanzi. Mnamo mwaka 1942, alihamishiwa mjini Dijon na kunako mwezi Novemba ya mwaka huo huo wa 1942 akahamishiwa mjini Lyon, Ufaransa, ambapo huko ndiko alikokuja kuwa kiongozi wa Gestapo ndogo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Makala kuhusu Barbie katika BBC
  2. http://www.archives.gov/iwg/research-papers/barbie-irr-file.html
  3. https://web.archive.org/web/20000816183001/http://www.time.com/time/magazine/1998/int/981109/latin_america.perons_na30a.html
  4. http://en.wikipedia.org/wiki/Stefano_Delle_Chiaie

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Klaus Barbie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.