Nenda kwa yaliyomo

Kizazi cha dhahabu cha hip hop

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Run-DMC na Beastie Boys katika picha ya vyombo vya habari iliyotolewa kwa ajili ya ziara yao ya Together Forever mwaka 1987.

Kizazi cha dhahabu cha hip hop ni jina la kutaja enzi ya dhahabu katika anga la muziki wa hip hop ulioundwa katikati au mwishoni mwa miaka ya 1980—hadi mwanzoni au katikati mwa miaka ya 1990.[1] [2][3][4]Wanaotajwa kuwa miongoni mwa kizazi hiki walitokea mjini New York. Wakaipa jina la new-school, huku ikichukua sura mpya kabisa kuanzia ubora, ubunifu, na ushawishi wake katika hip hop kwa ujumla baada ya aina hiyo kujitokeza na kuimarika katika enzi ya old-school. Pia, inahusiana na maendeleo na mafanikio ya hip hop kama tasnia kuu ya muziki.

Mada zilikuwa za aina mbalimbali, huku muziki ukijaribu mitindo mipya na kutumia sampuli kutoka kwa rekodi za zamani ili kuleta mtazamo mpana na tofauti.

Wasanii wanaohesabiwa kuwa hasa ni wa kizazi hiki ni pamoja LL Cool J, Slick Rick, Ultramagnetic MC's,Jungle Brothers, Run-DMC, Public Enemy, Beastie Boys, KRS-One, DJ Jazzy Jeff & the Fresh Prince, Eric B. & Rakim, De La Soul, Big Daddy Kane, EPMD, Biz Markie, Salt-N-Pepa, Queen Latifah, Gang Starr, na A Tribe Called Quest.

Albamu na nyimbo za wasanii hawa ziliibuka sambamba na zile za wasanii wa awali wa gangsta rap kama Schoolly D, Ice-T, Geto Boys, na N.W.A, pamoja na muziki wa kimahaba wa 2 Live Crew na Too Short, pamoja na muziki wa amsha-amsha kutoka kwa wasanii kama Fat Boys, MC Hammer, na Vanilla Ice.[5][6][7]

Orodha ya wasanii

[hariri | hariri chanzo]
Wasanii wa zama za dhahabu ya Hip Hop
Jina la Msanii Anapotoka Albamu Maarufu Wimbo Maarufu Mwaka
LL Cool J Queens, New York Radio, Bigger and Deffer "Mama Said Knock You Out" 1985–sasa
Slick Rick The Bronx, New York The Great Adventures of Slick Rick "Children’s Story" 1985–sasa
Ultramagnetic MCs The Bronx, New York Critical Beatdown "Ego Trippin’" 1984–sasa
Jungle Brothers New York City Straight Out the Jungle "I'll House You" 1986–sasa
Run-DMC Queens, New York Raising Hell "Walk This Way" 1983–2002
Public Enemy Long Island, New York It Takes a Nation of Millions to Hold Us Back "Fight the Power" 1985–sasa
Beastie Boys New York City Licensed to Ill "Sabotage" 1981–2012
KRS-One The Bronx, New York Criminal Minded "Sound of da Police" 1986–sasa
DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince Philadelphia, Pennsylvania He's the DJ, I'm the Rapper "Summertime" 1985–sasa
Eric B. & Rakim New York City Paid in Full "Eric B. Is President" 1986–1993
De La Soul Long Island, New York 3 Feet High and Rising "Me Myself and I" 1987–sasa
Big Daddy Kane Brooklyn, New York Long Live the Kane "Ain't No Half-Steppin'" 1986–sasa
EPMD Brentwood, New York Strictly Business "You Gots to Chill" 1987–sasa
Biz Markie Harlem, New York Goin' Off "Just a Friend" 1985–2021
Salt-N-Pepa Queens, New York Hot, Cool & Vicious "Push It" 1985–sasa
Queen Latifah Newark, New Jersey All Hail the Queen "U.N.I.T.Y." 1988–sasa
Gang Starr Brooklyn, New York Step in the Arena "Mass Appeal" 1985–2010
A Tribe Called Quest Queens, New York The Low End Theory "Can I Kick It?" 1985–2017
Schoolly D Philadelphia, Pennsylvania Schoolly D "P.S.K. What Does It Mean?" 1984–sasa
Ice-T Newark, New Jersey Rhyme Pays "6 'N the Mornin'" 1982–sasa
Geto Boys Houston, Texas We Can't Be Stopped "Mind Playing Tricks on Me" 1986–2005
N.W.A Compton, California Straight Outta Compton "Fuck tha Police" 1986–1991
2 Live Crew Miami, Florida As Nasty As They Wanna Be "Me So Horny" 1984–sasa
Too Short Oakland, California Born to Mack "Blow the Whistle" 1983–sasa
Fat Boys Brooklyn, New York Fat Boys "Wipeout" 1982–1991
MC Hammer Oakland, California Please Hammer Don't Hurt 'Em "U Can't Touch This" 1985–sasa
Vanilla Ice Dallas, Texas To the Extreme "Ice Ice Baby" 1989–sasa
Big L Harlem, New York Lifestylez ov da Poor & Dangerous "Put It On" 1992–1999
Kool G Rap & DJ Polo Queens, New York Road to the Riches "Ill Street Blues" 1986–sasa
Boogie Down Productions The Bronx, New York By All Means Necessary "My Philosophy" 1986–1992
Heavy D & The Boyz Mount Vernon, New York Big Tyme "Now That We Found Love" 1986–2011
Digital Underground Oakland, California Sex Packets "The Humpty Dance" 1987–2008
  1. "Golden Age Music Style Overview". AllMusic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-09.
  2. Carl Stoffers (2015-11-27). "Hip hop's golden age: Where are they now?". New York Daily News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-02-09.
  3. Hess, Mickey., 2007, Icons of Hip Hop [Two Volumes] [2 volumes]: An Encyclopedia of the Movement, Music, and Culture (Greenwood Icons), Greenwood Publishing Group, p. 341.
  4. Duinker, Ben; Martin, Denis (2017-09-26). "In Search of the Golden Age Hip-Hop Sound (1986–1996)". Empirical Musicology Review (kwa Kiingereza). 12 (1–2): 80–100. doi:10.18061/emr.v12i1-2.5410. ISSN 1559-5749.
  5. Bakari Kitwana (2005-06-21). "The Cotton Club". The Village Voice (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-02-09.
  6. Dan Epstein (2016-10-18). "'Cool as Ice': The Story Behind Vanilla Ice's Career-Killing Movie". Rolling Stone (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-02-09.
  7. "www.usatoday.com - Spin magazine picks Radiohead CD as best". www.usatoday.com. Iliwekwa mnamo 2025-02-09.