Nenda kwa yaliyomo

Kizambarau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kizambarau
Kizambarau wa kawaida (Amblyodipsas polylepis)
Kizambarau wa kawaida (Amblyodipsas polylepis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Fitzinger, 1843
Nusufamilia: Aparallactinae (Nyoka wanaofanana na matandu)
Bourgeois, 1968
Jenasi: Amblyodipsas
Ngazi za chini

Spishi 9:

Vizambarau ni nyoka wenye sumu wa jenasi Amblyodipsas katika familia Lamprophiidae. Asili ya jina lao ni rangi yao.

Nyoka hawa ni warefu kiasi, zaidi m moja kwa kipeo lakini chini ya sm 60 kwa kawaida. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia yenye mng'ao zambarau, hasa wakiwa wameambua ngozi hivi karibuni. Pengine rangi ya tumbo ni pinki au hudhurungi na spishi kadhaa zina milia njano.

Vizambarau huchimba ndani ya ardhi lakini wanaweza kuwinda juu ya ardhi. Hula nyoka wengine, mijusi na mijusi-nyungunyungu.

Chonge ni meno marefu ya nyuma yenye mifuo. Nyoka hawa wanaweza kung'ata lakini hakuna ripoti za dalili za kusumu katika watu. Hata hivyo wanafanana na nyoka wachimbaji na kwa hiyo jitahadhari.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kizambarau kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.