Kituo cha transfoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kituo cha 115 kV hadi 41.6/12.47 kV 5000 kVA 60 Hz chenye swichi ya saketi, vidhibiti, vifunga tena na jengo la kudhibiti mitambo.

Kituo cha transfoma (kwa ing. electrical substation) ni kituo tanzu katika mfumo wa kuzalisha na kusambaza umeme ambapo volteji inabadilishwa kutoka juu hadi chini au kinyume chake kwa kutumia transfoma[1]. Nishati ya umeme inaweza kutiririka kupitia vituo vya transfoma kadhaa kati ya kituo cha kuzalisha kwa upande mmoja na watumiaji kwa upande mwingine. Humo volteji ya umeme unaweza kubadilishwa mara kadhaa.

Ilhali umeme hufika kwa mtumiaji kama mkondo geu kwa volteji ya volti 230, unapitishwa kwenye nyaya kwa umbali mkubwa kwa umbo la mkondo mnyofu wenye volti elfu kadhaa. Kwa hiyo vituo vya transfoma vinahitajika kubadilisha mkondo wa umeme kutoka volteji ya juu kwa umbali mkubwa hadi volteji ya kati kwa umbali mdogo hadi volteji ya V 230 kwa matumizi ya nyumbani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Joint Consultation Paper: Western Metropolitan Melbourne Transmission Connection and Subtransmission Capacity". Jemena. Powercor Australia, Jemena, Australian Energy Market Operator. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-09. Iliwekwa mnamo 4 February 2016.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)