Nenda kwa yaliyomo

Kitambaa cha Akwete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamke wa Nigeria akisuka kwa mikono kitambaa cha akwete

Kitambaa cha Akwete ni kitambaa kinachosukwa kwa mikono kinachozalishwa katika eneo la Waigbo, ambacho mji wa Akwete unaofahamika pia kama Ndoki ambao kitambaa hiki kilipata jina lake, huko katika Jimbo la Abia, Nigeria umejulikana sana kwa utengenezaji wake.[1][2] Majina mbadala ni pamoja na Aruru maana yake kitu kilichosukwa, Mkpuru Akwete, Akuraku na kitambaa cha Akwete.[3] Ufumaji huu wa kitamaduni wa watu wa Igbo husuka katani, ukindu, pamba au nyuzi zingine kuwa bidhaa zilizokamilika.[4] Wakati vifaa vikali vya ukindu hutumika kwenye ngoma za jadi na hapo zamani kama kofia za kivita kwa mashujaa, miongoni mwa matumizi mengine, vifaa vya katani vilitumiwa kufuma taulo, kamba na mikoba. Pamba iliyosokotwa, ambayo ni laini na yenye rangi nyingi hutumika kusuka nguo za kuvaa kila siku. Vitambaa vya Akwete vina nakshi nyingi. Leo hii, wanawake wa Ndoki wanaendelea kutengeneza kitambaa cha Akwete kwa soko pana la kimataifa.[5]

  1. Obi-Young, Otosirieze. "The Women Weavers of Akwete". Folio Nigeria. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Chuku, Gloria (2013). Igbo women and economic transformation in Southeastern Nigeria, 1900-1960. London: Routledge. ISBN 978-0-415-64842-4. OCLC 812070253.
  3. "Akwete | Fashion History Timeline". fashionhistory.fitnyc.edu (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  4. Akwete cloth: An Igbo textile art Vanguard Newspaper JULY 26, 2012
  5. Indigenous African enterprise: the Igbo traditional business school (I-TBS). Ogechi Adeola. Bingley: Emerald Publishing Limited. 2020. ku. 167–175. ISBN 978-1-83909-033-2. OCLC 1225193026.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitambaa cha Akwete kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.