Songo Mnara
9°04′13″S 39°34′58″E / 9.0704°S 39.58288°E
Songo Mnara (pia: Songa Mnara, Songa Manara) ni kisiwa katika funguvisiwa la Kilwa, upande wa kusini mwa Kilwa Kisiwani. Kiutawala ni sehemu ya kata ya Pande Mikoma kwenye Wilaya ya Kilwa, Tanzania.
Upande wa mashariki wa kisiwa kuna maghofu ya mji wa kale wa Songo Mnara. Maghofu hayo yamekubaliwa pamoja na yale ya Kilwa Kisiwani katika orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale katika pwani ya Bahari ya Hindi.
Katika karne za 13 - 16 ilikuwa mji muhimu wa biashara ya Bahari Hindi kama inavyojulikana kutokana na mabaki ya bidhaa yaliyopatikana huko[1]. Mabaki ya dhahabu, fedha, lulu, marashi, vyombo vya Uajemi na kauri za China yalipatikana na kuonyesha upana wa biashara ya wenyeji[2].
Wataalamu wa akiolojia walitambua misikiti 6, makaburi 4, nyanja 3 na nyumba zaidi ya 20. Ujenzi ulikuwa wa matumbawe na simiti.[3]
Haijulikani ni nini iliyosababisha kuanguka kwa mji huo lakini kuna dalili za kuwa mwisho wa mji hulingana takriban na wakati wa kufika kwa Wareno katika Afrika ya Mashariki, hivyo kuna watalaamu wanaohisi mvurugo uliosababishwa na kufika kwa Wareno ulileta pia anguko la Songo Mnara.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya visiwa vya Tanzania
- Orodha ya miji ya kale ya Waswahili
- Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya Tanzania
- Orodha ya Urithi wa Dunia katika Afrika
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ndani ya jengo kuu
-
Jengo kuu
-
Mihrabu ya msikiti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stoetzel, Jack (2011). "Field Report: Archaeological Survey of Songo Mnara Island". Nyame Akuma. 76: 9–14.
- ↑ Zhao, Bing (Machi 2012). "Global Trade and Swahili Cosmopolitan Material Culture: Chinese-Style Ceramic Shards from Sane ya Kati and Songo Mnara (Kilwa, ,Tanzania)". Journal of World History. 23: 41–85. doi:10.1353/jwh.2012.0018.
{{cite journal}}
:|access-date=
requires|url=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fleisher, Jeffrey; Wynne-Jones, Stephanie (2012). "Finding Meaning in Ancient Swahili Spatial Practices". African Archaeological Review. 29: 171–207. doi:10.1007/s10437-012-9121-0.
{{cite journal}}
:|access-date=
requires|url=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara, maelezo kwenye tovuti ya UNESCO]
- Archaeology Magazine article on Songo Mnara
- Geonames.org
Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania | ||
---|---|---|
Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kinjumbi | Kipatimu | Kiranjeranje | Kivinje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Masoko | Miguruwe | Mingumbi | Miteja | Mitole | Namayuni | Nanjirinji | Njinjo | Pande | Somanga | Songosongo | Tingi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Songo Mnara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |