Mdiria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kisharifu)
Mdiria
Mdiria buluu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Coraciiformes (Ndege kama viogajivu)
Familia: Alcedinidae (Ndege walio na mnasaba na midiria)
Nusufamilia: Alcedininae (Ndege walio na mnasaba na midiria)
Jenasi: Alcedo Linnaeus, 1758

Ceyx Lacépède, 1799
Ispidina Cassin, 1856

Midiria ni ndege wadogo wa nusufamilia Alcedininae katika familia Alcedinidae. Spishi nyingine zinaitwa kizamiadagaa au kisharifu. Spishi zote zina rangi buluu mgongoni na kichwani, na tumbo ni jekundu kwa kawaida. Ndege hawa wana domo kubwa kwa kulinganisha na ukubwa wao ambalo lina ncha kali. Hukamata samaki wakipiga mbizi majini lakini hula gegereka na wadudu pia. Visharifu hula wadudu tu. Dume na jike pamoja huchimba tundu katika ukingo wa mto au uso mwingine wa wima wa mchanga. Tundu hili lina urefu wa mita 0.5-1 na jike huyataga mayai 2-10 kwenye mwisho wake uliokuzwa.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]