Nenda kwa yaliyomo

Kirekebisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
San Bonaventura al Palatino, kitovu cha "Riformella".
Mt. Leonardo wa Portomaurizio, tunda bora la "Riformella".

Kirekebisho (kwa Kiitalia: Riformella) kilikuwa juhudi za urekebisho zilizoanzishwa na Bonaventura wa Barcelona kati ya Ndugu Wadogo Wareformati wa kanda ya Roma katika nusu ya pili ya karne ya 17. Mwaka 1897 kiliunganika tena na shirika lote.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Miguel Bautista Gran, Mhispania mjane, mwaka 1640 alijiunga wa utawa wa Kifransisko kama bradha kwa jina la Bonaventura. Mwaka 1656 alikwenda kuishi upwekeni zaidi [1]. Mwaka 1658 alikubaliwa na kardinali Francesco Barberini kuhamia Roma akiwa na nia ya kueneza mtindo huo ili kuchochea bidii shirikani.

Bila kujali upinzani, alifaulu kuongea na Papa Aleksanda VII [2] akakubaliwa naye kwa hati Ecclesiae catholicae regimini ya tarehe 30 Agosti 1662 [2].

Wafuasi walitakiwa kutii viongozi wa shirika, nao walitakiwa kuanzisha nyumba za upwekeni katika kila kanda.[3] Kwa kuwa waliovutiwa waliongezeka haraka, ilibidi zianzishwe nyumba nyingi zaidi, hata mjini Roma, kwenye kanisa la San Sebastiano al Palatino, tarehe 12 Desemba 1677: konventi hiyo mpya ikawa kitovu cha Kirekebisho. Mwanzilishi alihamia huko hadi alipofariki tarehe 11 Septemba 1684.[2]

Huko Firenze, konventi ilianzishwa na Leonardo wa Portomaurizio mwaka 1709.[4]

Mwaka 1773, baada ya Wajesuiti kusambaratishwa, Wafransisko wa Kirekebisho wa San Bonaventura al Palatino walikabidhiwa kazi ya kuhubiri mafungo kwa wakleri wa Roma na wiki za uamsho katika maeneo ya kandokando.[4]

Mwaka 1821 atakayekuwa Papa Pius IX alijiunga na Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko katika kanisa hilohilo.[5]

Mwaka 1845 Wafransisko wa Kirekebisho walipewa uhuru mkubwa zaidi chini tu ya mtumishi mkuu wa Waoservanti.[4]

Kwa hati Felicitate quadam ya mwaka 1897, Papa Leo XIII aliunganisha kikamilifu matawi yote ya Ndugu Wadogo, likiwemo la Kirekebisho, isipokuwa Wakonventuali na Wakapuchini.[5]

Jumuia za "riformella" zilishika sana kanuni ya Kifransisko, hasa ufukara, walisali Liturujia ya Vipindi wakiiongezea saa 3 za sala ya moyo, walifunga miezi 8 kwa mwaka, walilala juu ya nyasi tu na kuvaa nguo ngumu sana.[4]

  1. Raimondo Sbardella, DIP, vol. I (1974), col. 1509.
  2. 2.0 2.1 2.2 Raimondo Sbardella, DIP, vol. I (1974), col. 1511.
  3. Raimondo Sbardella, DIP, vol. VII (1983), col. 1764.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Raimondo Sbardella, DIP, vol. VII (1983), col. 1765.
  5. 5.0 5.1 Raimondo Sbardella, DIP, vol. VII (1983), col. 1766.
  • Guerrino Pelliccia e Giancarlo Rocca (curr.), Dizionario degli Istituti di Perfezione (DIP), 10 voll., Edizioni paoline, Milano 1974-2003.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kirekebisho kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.