Kirai
Kirai ni kipashio cha muundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.
Muundo wa kiima na kiarifu ni ule ambao unahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa na ambao ndio muundo wa msingi katika lugha yoyote ile. Kiima hukaliwa na nomino kama neno kuu na kiarifu hukaliwa na kitenzi kama neno kuu.
Sifa za kirai
[hariri | hariri chanzo]Kirai hakina muundo wa kiima na kiarifu ambao unahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.
Uainishaji wa aina za virai hutegemea mahusiano maalumu baina ya maneno na neno kuu, kwa mfano neno kuu katika kirai nomino ni nomino.
Kirai na tungo yaani haina mojawapo ya tungo ambayo tungo nyingine ni neno kishazi na sentensi.
Kirai kikamilishi maana labda ni jibu.
Kirai huweza kutokea upande wa kiima au kiarifu katika sentensi.
Kirai ni kikubwa kuliko neno lakini kidogo kuliko kishazi.
Aina za virai
[hariri | hariri chanzo]- kirai nomino au kikundi nomino (RN): ni neno moja au zaidi ambayo yanafanya kazi ya nomino yaani kutaja mtu, kitu, mahali au hali. Neno kuu katika kirai ni nomino.
- kirai kitenzi (RT): ni kipashio cha lugha ambacho kinafanya kazi ya kitenzi yaani kuelezea kitendo ndani ya tungo. kirai kitenzi kinaweza kuundwa kwa neno moja au zaidi.
- kirai kielezi (RE): ni neno moja au zaidi ambayo yanafanya kazi ya kielezi yaani kutoa taarifa zaidi kuhusu kitenzi au tendo; kirai kielezi hutoa taarifa zinazojibu maswali kama vile lini, wapi, vipi, na mara ngapi?
- kirai kivumishi (RV): ni maneno yanayofanya kazi ya kivumishi yaani yanatoa taarifa zaidi kuhusu kivumishi; neno kuu ndani ya kirai hiki ni kivumishi. Mara nyingi kirai kivumishi huwa sehemu ya kirai nomino. Mfano: mwanafunzi mkimya zaidi amekuwa wa kwanza.
- kirai kiunganishi (RU): ni kirai ambacho neno linalotawala ndani yake ni kiunganishi. Kwa kawaida kiunganishi hicho hufuatiwa na kirai nomino. Mifano:
- ameweka juu ya meza
- ameandika kwa kalamu
- amesafiri kwa ndege
- kirai kihusishi (RH): ni kirai ambacho neno linalotawala ndani yake ni kihusishi. Kwa kawaida kihusishi hicho hufuatiwa na kirai nomino.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kirai kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |