Kipulaar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kipulaar ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Senegal, Gambia, Guinea-Bisau, Mauritania, Mali na Guinea inayozungumzwa na Wafulfulde. Isichanganywe na lugha ya Kipular ambayo pia ni lugha ya Senegal. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kipulaar nchini Senegal imehesabiwa kuwa watu 2,740,000. Pia kuna wasemaji 295,000 nchini Gambia, 265,000 nchini Guinea-Bisau, 192,000 nchini Mauritania, 175,000 nchini Mali na 24,000 nchini Guinea. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipulaar iko katika kundi la Kiatlantiki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kipulaar kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.