Kimbonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimbonga (au Kimboa) ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wambonga. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimbonga imehesabiwa kuwa watu 1490. Lakini Blench (2011) amedai kuwa hakuna wasemaji wa Kimbonga kama lugha ya kwanza. Kwa hiyo inawezekana kuwa lugha imeshatoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimbonga iko katika kundi la Kijarawan ambalo linafanana na lugha za Kibantu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimbonga kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.