Kilufu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilufu ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Walufu. Mwaka wa 2006 idadi ya Walufu imehesabiwa kuwa watu 3200 lakini wengi wao wamebadilisha lugha kuongea Kijukun. Kwa vile hasa ni wazee tu ambao wameendelea kuongea Kilufu inawezekana kwamba Kilufu kitatoweka hivi karibuni. Ingawa uainishaji wa lugha ya Kilufu kwa ndani zaidi haujulikani, imesemekana kuwa ilifanana na lugha ya Kibete ambayo ni katika kundi la Kijukunoidi linalofanana na lugha za Kibantu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilufu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.