Nenda kwa yaliyomo

Kilima cha Hyrax

Mary na Louis Leakey.

Kilima cha Hyrax ni eneo la kihistoria karibu na ziwa Nakuru katika Bonde la Ufa nchini Kenya. Inachukuliwa kama mojawapo kati ya maeneo muhimu zaidi ya Neolithiki nchini Kenya. Kilima cha Hyrax kiligunduliwa na Louis Leakey na Mary Leakey mwaka wa 1926.

Uchimbaji ulianza mwaka wa 1937, ukiongozwa na Mary Leakey. Mabaki ya makazi, makaburi na ngome zilizojengwa kwa mawe yalipatikana, pamoja na viwiliwili 19, ambayo hayakuwa na vichwa na katika mwima uliyojikunja. Pia bodi la Bao lilipatikana, pamoja na alama ambazo zilikuwa zimekwizha andikwa. Jumba dogo la Makumbusho huonyesha matokeo kutoka enzi ya kitmabo ya zama za Chuma.

Kilima cha Hyrax ni mojawapo kati ya maeneo ambayo hupatikana karibu na mashimo ya Sirikwa.

    0°16′53″S 36°6′18″E / 0.28139°S 36.10500°E / -0.28139; 36.10500