Kilatini
Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule na vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Kilatini ilikuwa lugha hai takriban kati ya 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake ziliendelea kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi.
Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa wikipedia.
Kilikuwa
- lugha ya Dola la Roma (angalia pia Roma ya Kale)
- lugha mama ya lugha za Kirumi kama Kiitalia, Kihispania, Kireno, Kifaransa na Kiromania
- lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi
- lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi za Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mwaka 476 BK hadi mnamo 1700 BK
- lugha pekee ya liturgia katika Kanisa la Kilatini hadi 1965
Hadi leo ni
- lugha ya kidini katika Kanisa Katoliki
- lugha rasmi katika nchi ya Vatikano
Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya kama lugha ya kigeni.
Kiswahili kimerithi maneno ya asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia sitini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.
Kilatini huendelezwa na kukuzwa na wapenzi wa lugha. Kuna misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k.. Wikipedia ya Kilatini ina makala zaidi ya 54,000.
Tazama pia
Viungo vya nje
- makala za OLAC kuhusu Kilatini
- lugha ya Kilatini katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/lat
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kilatini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kilatini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |