Nenda kwa yaliyomo

Kikirigizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kikirigizi ni lugha ya Kiturki nchini Kirgizia, Uchina, Afghanistan, Urusi, Uturuki na Uzbekistan inayozungumzwa na Wakirgizi. Kikirigizi ni lugha rasmi katika nchi za Kirgizia. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kikirigizi nchini Kirgizistan imehesabiwa kuwa watu 3,830,000. Pia kuna wasemaji 160,000 nchini Uchina (2000), 60,100 nchini Tajikistan (2012) na 750 nchini Afghanistan (2000). Idadi za wasemaji wa Kikirigizi nchini Uturuki, Uzbekistan na Urusi hazijulikani. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikirigizi iko katika kundi la Kiturki ya Magharibi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikirigizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.