Kichapuzi chembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la CERN kutoka hewani

Kichapuzi chembe (kikamilifu zaidi Kichapuzi cha chembe cha nyuklia: kwa Kiingereza particle accelerator) ni kifaa cha kuongezea mwendo wa chembe za nyuklia, yaani chembe ndogo sana, kama atomu au sehemu za atomu.

Mfano maarufu ni Kichapuzi chembe kiitwacho CERN kilichojengwa karibu na mji wa Geneva, mpakani kwa Uswisi na Ufaransa.

Kichapuzi chembe kinaharakisha mwendo wa chembe hadi kufikia kasi ya juu na kukaribia kasi ya nuru. Kichapuzi kinatekeleza kazi hii kwa kutumia uga sumakuumeme zinazosukuma chembe kama elektroni, protoni au viini vya atomi. Matumizi ya vichapuzi chembe ni hasa utafiti wa fizikia ya chembe. Lakini mashine hizi zinatumiwa pia kwa tiba ya kansa kwa kulenga nyutroni kwa seli husika[1].[2]

Vichapuzi chembe vinakuwa kubwa zaidi kadiri chembe zinazochunguliwa zilivyo ndogo zaidi. Mashine kubwa sana kama vile CERN huko Geneva zinatumiwa kwa kutafuta chembe ambazo ni ndogo kuliko atomi. Mashine ndogo hutumiwa kwa utafiti kwa kiini cha atomi au kwa tiba.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. U. Amaldi and G. Kraft, "Radiotherapy with beams of carbon ions" in Rep. Progr. Physics 68 (2005) [pp.?] 1861, 1861–1882.
  2. Marcos d’Ávila Nunes, Protontherapy Versus Carbon Ion Therapy: Advantages, Disadvantages and Similarities, Springer 2015 , uk 21ff; iliangaliwa kupitia google books tar. 9-12-2016
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kichapuzi chembe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.