Nenda kwa yaliyomo

Kigavi umeme

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kigavi umeme cha ATX kikiwa kimeondolewa kifuniko cha juu.

Kigavi umeme (kwa Kiingereza: Power Supply Unit - PSU) ni kifaa kinachobadilisha umeme wa AC (Alternating Current) kutoka kwenye plagi ya ukutani na kuubadilisha kuwa umeme wa DC (Direct Current) wa volti ya chini. Umeme huu wa DC ndio unaotumika kuendesha vijenzi vya ndani vya kompyuta ya mezani. Kompyuta za kisasa hutumia kigavi umeme kinachoitwa 'switched-mode power supplies'. Baadhi ya Kigavi umeme huwa na swichi ya kubadilisha volti, huku vingine vikijirekebisha moja kwa moja kulingana na volti kuu.

Vigavi umeme vingi vya kompyuta za mezani vya kisasa vinafuata vipimo vya ATX. Vipimo hivi vinajumuisha ukubwa na viwango vya volti. Wakati Kigavi umeme cha ATX kimeunganishwa kwenye umeme wa kawaida (mains), huendelea kutoa volti ya kusubiri ya 5-volt (5VSB). Volti hii inaruhusu vipengele fulani vya kompyuta na vifaa vingine kuendelea kupata umeme hata kompyuta ikiwa imezimwa (standby). Kigavi umeme cha ATX huwashwa na kuzimwa kwa kutumia ishara kutoka kwenye bodimama. Pia hutoa ishara kwa bodimama kuonyesha kuwa volti za DC ziko sahihi, hivyo kuwezesha kompyuta kuwasha na kuanza kazi kwa usalama. Kiwango kipya zaidi cha ATX PSU ni toleo la 3.0, lililotolewa katikati ya mwaka 2024.

Mchoro wa mzunguko ulio rahisishwa wa PSU ya kawaida
Mchoro wa saketi ya kudhibiti volti wa XT na AT
Internals of a PSU with passive PFC (left) and active PFC (right)

Kazi kuu ya Kigavi umeme ni kubadilisha mkondo wa umeme mbadala (AC) kutoka soketi ya ukutani kwenda kwenye mkondo wa umeme wa moja kwa moja (DC). Umeme huu wa DC ndio unaotumika kuendesha motherboard, prosesa, na vifaa vingine vilivyounganishwa kwenye kompyuta. Volti kadhaa za DC zinahitajika, na ni lazima zidhibitiwe kwa usahihi ili kuhakikisha kompyuta inafanya kazi vizuri. "Njia ya usambazaji wa umeme" au "njia ya volti" inahusu volti maalum inayotolewa na Kigavi umeme.[1]

Baadhi ya Vigavi umeme vinaweza pia kutoa volti ya kusubiri. Hii inaruhusu sehemu kubwa ya mfumo wa kompyuta kuzimwa baada ya kujiandaa kwa ajili ya kulala (hibernation) au kuzima kabisa, na kuwashwa tena na tukio fulani. Umeme wa kusubiri unawezesha kompyuta kuwashwa kwa mbali kupitia wake-on-LAN na Wake-on-ring au ndani kwa kutumia Keyboard Power ON (KBPO), ikiwa motherboard inaiunga mkono. Volti hii ya kusubiri inaweza kuzalishwa na kifaa kidogo cha usambazaji wa umeme cha linear ndani ya kitengo au kifaa cha usambazaji wa umeme cha kubadilisha, ambacho hushiriki baadhi ya vijenzi na kitengo kikuu ili kuokoa gharama na nishati.

  1. Woligroski, Don (Desemba 14, 2011). "Power Supply 101: A Reference Of Specifications". Tom's Hardware. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 23, 2018. Iliwekwa mnamo Julai 12, 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.