Nenda kwa yaliyomo

Kidudu-kifuko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidudu-kifuko
Kidudu-kifuko (Symbion pandora): kushoto - hatua ya kujilisha na lava aliyeambatishwa, kulia - lava kubwa zaidi
Kidudu-kifuko (Symbion pandora): kushoto - hatua ya kujilisha na lava aliyeambatishwa, kulia - lava kubwa zaidi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Platyzoa
Faila: Cycliophora
Funch & Kristensen, 1995
Ngeli: Eucycliophora
Oda: Symbiida
Familia: Symbiidae
Jenasi: Symbion
Funch & Kristensen, 1995
Ngazi za chini

Spishi 3:

Vidudu-kifuko ni vidudu wadogo sana wa faila Cycliophora wanaoishi kwenye sehemu za mdomo za kambamawe. Hadi sasa wamefunua kwenye spishi tatu za kambamawe: kambamawe wa Marekani (Homarus americanus), kambamawe wa Ulaya (Homarus gammarus) na kambamawe wa Unowe (Nephrops norvegicus)[1].

Mchoro wa Symbion pandora ukionyesha mwili kama kifuko, mpare wa mdomo wenye minyiri, mkundu, sahani ya kujiambatisha na lava aliyeambatishwa kando.

Wapevu hutokea katika hatua mbili. Ile kubwa zaidi ni hatua ya kujilisha, ambayo ina urefu wa µm 350 na upana wa µm 120. Ina mwili unaofanana na kifuko na mdomo wenye mpare unaobeba minyiri na mkundu juu yake (tazama mchoro). Inashikamana na unywele wa kambamawe kwa njia ya sahani ya kunyonya. Katika hatua hii wanyama wanaweza kuzaa bila utungisho kwa kuchipua nakala za wenyewe[2].

Katika hatua ya ngono kuna jinsia mbili ambazo zote zina urefu wa µm 85 na upana wa µm 40. Dume hana mdomo, mkundu wala mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, lakini ana korodani mbili. Jike ana mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na yai moja. Baada ya utungisho, yai hukua na kuwa lava ambaye hufyonza mwili wa mama yake hadi ganda tu libaki. Kisha lava huogelea kwenda kutafuta mwenyeji mpya[2].

  1. Marshall, Michael (28 Aprili 2010). "Zoologger: The most bizarre life story on Earth?". New Scientist. Iliwekwa mnamo 19 Novemba 2018. ... In 1995, Peter Funch and Reinhardt Møbjerg Kristensen, both then at the University of Copenhagen, Denmark, discovered an animal so unlike any other that a new phylum – Cycliophora – had to be created just for it. ...{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 P. Funch & R. M. Kristensen (1995). "Cycliophora is a new phylum with affinities to Entoprocta and Ectoprocta". Nature. 378 (6558): 711–714. Bibcode:1995Natur.378..711F. doi:10.1038/378711a0. S2CID 4265849.