Nenda kwa yaliyomo

Kichwa cha Bronzi kutoka Ife

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichwa cha Ife kinachoonyeshwa katika Makumbusho ya Uingereza.

Kichwa cha Bronzi kutoka Ife au Kichwa cha Ife[1] ni moja ya sanamu kumi na nane za aloi ya shaba zilizogunduliwa mwaka 1938 huko Ife nchini Nigeria, kituo cha kidini na kifalme cha Wayoruba. Inaaminika kumwakilisha mfalme. Huenda ilitengenezwa katika karne ya 14–15 BK. Uhalisia na ufundi uliokamilika wa vitu hivyo ulipinga mitazamo ya kudharau na ya kimajivuno ya Magharibi kuhusu sanaa ya Afrika. Sifa za kiasili za vichwa vya Ife ni za kipekee, na kufanana kwa mitindo ya kazi hizi kunadokeza kuwa zilitengenezwa na msanii mmoja au katika warsa mmoja.[2][3][4][5]

  1. The name used by the British Museum
  2. The British Museum collection database "scope note" on "copper alloy", "brass" and "bronze" reads "The term copper alloy should be searched for full retrievals on objects made or bronze or brass. This is because bronze and brass have at times been used interchangeably in the old documentation, and copper alloy is the Broad Term of both. In addition, the public may refer to certain collections by their popular name, such as 'The Benin Bronzes' most of which are actually made of brass." British Museum, "Scope Note" for "copper alloy". Britishmuseum.org. Retrieved on 2014-05-26.
  3. Bronzes from Ife and Benin, Peter Herrmann, Berlin, 2007, retrieved 30 November 2013
  4. National Art Collections Fund. "Art we've helped buy". Art Fund. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-24. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Ife head Brass head of a ruler, British Museum highlights, retrieved 30 November 2013