Nenda kwa yaliyomo

Kibena (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibena ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wabena. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kibena imehesabiwa kuwa watu 670,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibena iko katika kundi la G60.

Lahaja[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na tahariri ya Dr. Kilemile (2009), Kibena ni lugha tajiri sana kwa maneno na ni pana sana ikiwa na lahaja kuu tano: Ki-Kilavwugi (Maeneo ya Ilembula); Kisovi (Kuanzia Lusisi hadi Makambako), Kimaswamu (Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu), Ki-Lupembe (Lupembe) na Kimavemba (Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi ambayo si ya Maswamu).

Lugha ni moja tu; tofauti ni ndogondogo, zikitokana na matamshi, mfano kukaza "dz", kwa lahaja zote isipokuwa Kikilavwugi ambacho ingawa inaandikwa "dzi" inatamkwa kama "dji" umuhudji; na Kilupembe inaandikwa "dzi" lakini watumiaji wanatamka kama "chi" umuhuchi, achile - amekuja, wakati "adjile" (Kikilawugi)... Wengine wote wanakaza adzile, umuhudzi. Tofauti nyingine ni ya kutumia k na h. Mfano: Kamwene/ Hamwene, Kangi/hangi, ukukulima/uhulima n.k.

Suala lingine ni tofauti ya baadhi ya maneno mfano: Asubuhi: Lwamilawu/palukela; Kuketi: kwikala/hwikala/ kutama; Chuma mboga: hukova/kukova imboga na huyava/kuyava imboga; Zizi la Ng'ombe: Ligoma na livaga; nyumbani: hukaye na hunyumba; habari za kazi: mwidaliha na madzengo nk.

Kamusi inatakiwa kujumuisha maneno yote yanayohitilafiana na kudokeza yanakotumika. Maana kamusi ni kihenge cha lugha. Hivyo kuita kamusi yale maneno machache ya Kibena aliyoorodhesha Dr. Joshua ni dhihaka kwa lugha hii ambayo ni tajiri mno kwa misamiati.

Kwa mfano neno kupiga tu lina maneno zaidi ya 100 yakionyesha huyo aliyepigwa amepigwa wapi na ku-suggest hali yake baada ya kupigwa. Pia huashiria hali ya mpigaji. Mfano: (tumia) "k" au "h" kutokana na eneo unalotoka: hutova(general) lakini: hupafula (kiganja), hupefula (nyuma ya kiganja), hututa, hukinya, hung'ilula; hung'alula, hutununa, huwindula, hupwinda, hupana, hulibinga, hufidula, hutadisa, hugong'ola, huniabula, hukinya, huhudugula, huniesa n.k.

Mfumo wa Sauti (Fonolojia)[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kibena ina irabu 5 na konsonanti 23. Pia, tofauti kati ya irabu fupi na irabu ndefu huleta tofauti za maana.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

  • Priebusch, Martin. 1935. Bena-Hehe-Grammatik. Berlin: Kommissionsverlag der Buchhandlung der Berliner Missionsgesellschaft.
  • Sowa, R. von. 1900. Skizze der Grammatik des Ki-Bena (Ki-Hehe) in Deutsch-Ostafrika. Zeitschrift für afrikanische und oceanische Sprachen, 5, uk. 63-75.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibena (Tanzania) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.