Nenda kwa yaliyomo

Khadra Haji Ismail Geid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Khadra Haji Ismail Geid (Kisomali: Khadra Xaaji Ismaaciil Geydh) ni mwanasiasa wa Somalia.

Mwaka 2011, alikua Meya wa mji wa Gabiley na kuwa mwanamke wa kwanza kuwa meya katika Somaliland. [1]Kwa sasa ni Naibu Meya wa Gabiley.

Geid alijiunga na chama tawala cha Amani, Umoja, and Maendeleo (Kulmiye) mwaka 2002.

Mnamo Mei 2011, aliidhinishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Meya wa Wilaya ya Gabiley. Alikuwa meya wa saba wa wilaya hiyo tangu mwaka 1991 na mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika Somaliland.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa meya, alihudumu miaka minne kama diwani wa halmashauri na miaka sita kama Naibu Meya.[2]

Mnamo 13 Machi 2012, aliondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani katika baraza la mji wa Gabiley, na baadaye akachaguliwa tena kuwa Naibu Meya.

  1. "Article on UNPO and the Uyghurs in Checks & Balances -" (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2009-11-02. Iliwekwa mnamo 2026-05-22.
  2. "Khadra Gaydh: The first" Madam Mayor" in Somaliland". Hiiraan Online (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-05-22.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khadra Haji Ismail Geid kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.