Kevin Großkreutz
| Kevin Großkreutz | |
| Amezaliwa | Kevin Großkreutz 19 Julai 1988 Dortmund, Ujerumani Magharibi |
|---|---|
| Nchi | Ujerumani |
| Urefu | 1.86 m |
Kevin Großkreutz (alizaliwa 19 Julai 1988) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Ujerumani anayecheza nafasi ya beki wa kulia na winga katika klabu ya TuS Eichlinghofen.
Alicheza mechi yake ya kwanza katika ngazi ya wakubwa akiwa na Rot Weiss Ahlen, na mnamo mwaka 2009 alijiunga na Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Bundesliga, akiichezea mechi 233 katika mashindano yote na kufunga mabao 27. Mafanikio yake wakati akiwa katika uwanja wa Westfalenstadion mji wa Dortmund nchini Ujerumani yalijumuisha mataji mawili mfululizo ya Bundesliga, ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa mara mbili kwa msimu mmoja mnamo mwaka 2012.[1]
Katikati ya mwaka 2015, baada ya kucheza mechi chache katika klabu ya Borussia Dortmund, Großkreutz alihamia klabu ya Süper Lig ya Galatasaray ambapo hakucheza mechi hata moja katika nusu ya msimu. Alirejea Bundesliga kwa kusaini mkataba na klabu VfB Stuttgart mnamo Januari 2016. Mnamo Machi 2017, mkataba wake ulisitishwa baada ya kuhusika katika ugomvi wa baa. Mwezi mmoja baadaye, alijiunga na klabu ya ligi daraja la pili ya Darmstadt 98. Baada ya msimu mmoja na Darmstadt 98, alikaa misimu miwili na KFC Uerdingen 05 katika ligi daraja la tatu kabla ya kujiunga na TuS Bövninghausen mnamo Januari 2021.
Akiwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani kati ya mwaka 2010 na 2014, alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2014.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kevin Großkreutz - DFB". DFB. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kevin Großkreutz - National Football Teams". National Football Teams. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kevin Großkreutz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |