Nenda kwa yaliyomo

Kesz Valdez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chris "Kesz" Valdez alizaliwa 26 Desemba 1998 ni mwanahisani kutoka Ufilipino na mwanzilishi wa Championing Community Children (C3). Akiwa na umri wa miaka 13, Kesz Valdez alitunukiwa tuzo ya kimataifa ya amani ya watoto ya mwaka 2012 huko The Hague, Uholanzi. Mchungaji Desmond Tutu, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, alimkabidhi Valdez tuzo hiyo tarehe 19 Septemba.[1]

Pia yeye ni mtu wa kwanza kutoka kusini mashariki mwa Asia kupokea tuzo ya kimataifa ya amani ya watoto na kwa sasa ndiye mdogo zaidi miongoni mwa waliowahi kuteuliwa kufikia hatua ya mwisho ya utambuzi huo.[2][3][4] Kiasi cha pesa cha Euro 100,000 ilitumika kufadhili miradi mbalimbali ya watoto na kuendeleza juhudi zake za kusaidia watoto wa Ufilipino.[5]

Akitoka katika familia maskini ,huku akiwa na dhamira ya kuleta maboresho kwa watoto wengine wa mitaani, Valdez akiwa bado mdogo aliangazia mateso yao katika jamii ya kimataifa. Juhudi zake kutambuliwa huko The Hague zilileta fahari kubwa kwa Baraza la Wawakilishi la Ufilipino kupitia azimio maalum.[6]

Valdez amezaliwa Imus, Cavite, Ufilipino tarehe 26 Desemba 1998. Akiwa na umri wa miaka miwili pekee, watu wangeweza kumkuta Kesz Valdez akichambua taka katika dampo maarufu la Captive huko Manila, jambo linaloonyesha jinsi maisha yake yalivyokuwa magumu tangu akiwa mdogo. Valdez alipigwa na baba yake na kutelekezwa na mama yake, hadi alipofikisha miaka minne baada ya wazazi wake kuamua kkumuasili. Kutokana na hali hiyo, alipata sifa mbaya na alilazimika kujitafutia mahitaji yake mwenyewe.

Kwa sababu ya hali ya nyumbani, alilazimika kuombaomba, kuokota taka, kula mabaki ya taka kama chakula, na kupeleka pesa ili kusaidia uraibu wa dawa za kulevya na pombe wa baba yake. Alitoroka familia yake iliyomtesa akiwa na miaka minne na alitumia siku zake kuomba chakula katika mitaa ya makazi duni zaidi ya Manila. Usiku, alipatikana akilala juu ya makaburi wazi au kwenye milango ya maduka. Kwa zaidi ya 1 12 miaka, Valdez alikuwa mtoto asiye na makazi aliyekosa mahali pa kudumu pa kuishi, kulala au kupata chakula. Baadaye alisoma katika kikundi cha msaada kiitwacho Club 8586 alipokuwa mkubwa kidogo. Valdez alilelewa na kupewa malezi pamoja na ushauri na Manalaysay baada ya kuungua vibaya alipoanguka kwenye moto. Manalaysay alikuwa mshauri wa mwanahisani mwingine anayefanya kazi na watoto wa mitaani, shujaa wa CNN Efren Peñaflorida.[7]

Mwaka 2006, Valdez pamoja na marafiki zake walianzisha jumuiya ya kutetea watoto iliyoitwa Championing Community Children, Kesz's Action.[8] Hili ni shirika linalolenga kutoa matumaini na kuwaonyesha watoto wa mitaani kwamba wanaweza kubadilisha maisha yao na kuwahamasisha wengine kufanya hivyo pia. Kupitia shirika lake, Valdez amesaidia zaidi ya watoto 10,000 katika jamii yake. Aliweza kuwahamasisha na kuwasaidia watoto wengi wadogo kupitia uzoefu wake binafsi wa maisha, jambo linaloonyesha jinsi alivyokuwa wa kipekee.[9] Shirika lake la Championing Community Children halifundishi tu usafi wa mwili bali pia hutoa mahitaji ya msingi kwa watoto wa makazi duni kama vile nguo, viatu vya wazi na vinyago.[10]

  1. Raftery, Isolde (26 Septemba 2012). "Former Filipino street kid, 13, wins International Children Peace Prize". NBC News. ku. NBC website. Iliwekwa mnamo Agosti 16, 2024.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Pinoy peace prize awardee Kesz Valdez dedicates award to guardian". GMA News. Septemba 25, 2012.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Young Pinoy peace awardee Kesz Valdez tells world's children: Do not lose hope". GMA News. Septemba 25, 2012.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "2012 – Kesz Valdez (13), Philippines". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-03-11.
  5. Pinoy peace prize awardee Kesz Valdez dedicates award to guardian
  6. Lapid, Manuel (2012). "PDF: The Fifteenth Congress of the Republic of Philippines - 3 regular session Congratulating K. Valdez" (PDF). The Fifteenth Congress of the Republic of Philippines - 3 Regular Session Congratulating K. Valdez: a pdf of the resolution 881 kutoka a pdf of the resolution 881.
  7. "Filipino kid wins $130,000 peace prize". Inquirer Global Nation. Septemba 22, 2012.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Yee, Jovic (Januari 16, 2016). "Award-winning street kid remains rooted to his past". Philippine Daily Inquirer. Iliwekwa mnamo Agosti 16, 2024.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Cris "Kesz" Valdez, 13-year-old boy, commended for winning 2012 International Children's Peace Prize". Remate. Desemba 10, 2012.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Medina, Sarah (Septemba 25, 2012). "Kesz Valdez: Homeless Filipino Boy Wins $130,000 Children's Peace Prize". HuffPost. Iliwekwa mnamo Agosti 16, 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)