Nenda kwa yaliyomo

Kate Yeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kate Yeo.

Kate Yeo (alizaliwa 2001) ni mwanaharakati wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi kutoka Singapuri.

Uharakati

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2018, Yeo alianzisha kampeni ya BYO Bottle SG ili kupinga matumizi ya plastiki zinazotumika mara moja nchini Singapuri.[1] Mpango huo umefanya kazi na vibanda vya vinywaji vyenye idadi ya 231 na kuwafikia karibu watu 10,000.[2][3] Alipata Tuzo ya pili katika mashindano ya Insha ya Kimataifa kwa Vijana ya mfuko wa Amani wa Goi hii ni kutokana na insha yake yenye kichwa "Mapambano Dhidi ya Uchafuzi wa Plastiki".

Yeo alikuwa mmoja wa waandaaji wa mandamano ya hali ya hewa ya We The Planet kwa Siku ya Dunia 2020.[4] Kisha alianzisha shirika la Mpango wa Kuanzisha Upya Dunia,ambalo ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa linaloongozwa na vijana linalojitahidi kufanya harakati za hali ya hewa zipatikane kwa wote.[5] Pia alisaidia kuandaa mkutano wa mazingira ya vijana mtandaoni, ulioandaliwa na wabunge wa vijana wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa.[6] Mnamo Aprili 2021, alikuwa mshiriki wa jopo katika mkutano wa Othering & Belonging, pamoja na mwandishi na mwanaharakati wa hali ya hewa Naomi Klein na watetezi wengine wa vijana Tokata Iron Eyes, Xiye Bastida na Samia Dumbuya.[7] Alihudhuria mkutano wa COP27 nchini Misri mwaka wa 2022 ili kuangalia jinsi biashara ya kimataifa ya mikopo ya kaboni itakavyotekelezwa.[8] Baada ya mkutano huo, alizungumzia kuhusu kuhisi kukatishwa tamaa kutokana na ukosefu wa maendeleo lakini akiendelea kuwa na  "tumaini lisiloelezeka".

Yeo pia ni mwanzilishi wa Yeo pia ni mwanzilishi wa kikundi cha Dartmouth Huru kutoka Mafuta ya Kisukuku, ambalo linataka Chuo cha Dartmouth kukata uhusiano wa kifedha na makampuni ya mafuta ya visukuku.[9] Mnamo Oktoba 2023, alishiriki katika kuandika ripoti inayokosoa uhusiano kati ya Taasisi ya Nishati na Jamii ya Arthur L. Irving na kampuni ya mafuta ya Irving. [10][11]

  1. Durva Simone Bose (2021-07-05). "Kate Yeo on championing the 'bring your own' movement". ZERRIN (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  2. "BYO Bottle SG". BYO Bottle SG (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  3. Jamie Mah (2021-06-23). "Singapore's sustainability: Our garden city's efforts". Hype Singapore (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  4. Seah, Kimberly (2020-12-30), "A Singapore Perspective: Is Activism Enough to Save the Climate? - The IAS Gazette", The IAS Gazette (kwa American English), iliwekwa mnamo 2025-11-14
  5. "The Re-Earth Initiative on Promoting Inclusivity, Accessibility & Unity in the Climate Change Movement". The Teen Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  6. Rebecca Williams (2020-11-27). "Kate Yeo: Plastics and Climate Youth Activist". EUI Environmental Law and Governance Blog (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  7. "Video & Recap: The 2021 O&B Virtual Summit | Othering & Belonging Institute". belonging.berkeley.edu. Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  8. "What S'pore youth want at COP27: Finalising carbon credits plan, financing for vulnerable nations", The Straits Times (kwa Kiingereza), 2022-11-06, ISSN 0585-3923, iliwekwa mnamo 2025-11-14
  9. Mara Hoplamazian (2023-10-24). "Dartmouth students urge college to stop accepting research money from fossil fuel companies". New Hampshire Public Radio (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  10. Cloe Logan (2023-10-24). "Students at this Ivy League school call out Irving Oil | Canada's National Observer: Climate News". www.nationalobserver.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  11. "Fossil Free Dartmouth publishes "Investigating Irving" report critiquing College's ties to fossil fuels". Fossil Free Dartmouth publishes “Investigating Irving” report critiquing College’s ties to fossil fuels - The Dartmouth (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.