Kassim Aidara
Kassim Aidara (alizaliwa tarehe 12 Mei 1987) ni mchezaji wa zamani wa soka la kulipwa mwenye uraia wa Senegali na Ufaransa ambaye alicheza kama kiungo.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Aidara alianza kusakata kandanda katika klabu ya Wellington United ya nchini Nyuzilandi , kisha akaziwakilisha klabu za ligi za chini nchini Ujerumani ambazo ni Niendorfer TSV, USC Paloma, na Lüneburger SK Hansa.
Mnamo Desemba 2011, Aidara alisaini mkataba na klabu ya Estonia ya Tallinna Kalev.[2] Baada ya kufunga mabao manne akiwa na klabu hiyo, tarehe 31 Julai 2012 alihamia Sillamäe Kalev ya nchi hiyo hiyo .[3] Katika msimu wa 2013, alifunga mabao 17 katika mechi 34. Alihamia FCI Tallinn mwaka uliofuata.[4] Mwishoni mwa mwaka huo, alifanya majaribio na klabu ya Vietnam Sông Lam Nghệ An.[5] Mwaka 2016, alirejea Sillamäe.[6]
Tarehe 4 Oktoba 2017 Aidara alibadilisha klabu na nchi na kusaini katika klabu ya Minerva Punjab inayoshiriki Ligi ya daraja la pili nchini uhindi.[7]Tarehe 25 Novemba, alicheza mechi yake ya kwanza kwa klabu hiyo katika sare ya 1–1 dhidi ya Mohun Bagan.[8] Tarehe 11 Desemba, alifunga bao lake la kwanza kwenye klabu hiyo katika ushindi wa 2–1 dhidi ya Chennai City.[9] Aidara alishinda Ligi ya daraja la pili msimu wa 2017–18 akiwa na Minerva Punjab.
Aidara alijiunga na East Bengal kwa msimu wa 2018–19 baada ya msimu wa Ligi ya daraja la pili 2017–18 kumalizika.
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Ni kaka yake Mohamed Aidara ambae pia ni mwanakandanda. [10]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mchezaji bora wa mwezi Meistriliiga: August 2013.[11]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Kassim Aidara » Profile". worldfootball.net (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-05.
- ↑ "DELFI VIDEO: Tallinna Kalevi ründaja unistab Senegali koondisse pääsemisest". Delfi Sport. Iliwekwa mnamo 2026-02-05.
- ↑ "Kassim Aidara", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2026-01-11, iliwekwa mnamo 2026-02-05