Nenda kwa yaliyomo

Kanisa la Kwanza la Wabaptisti nchini Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwonekano wa mbele wa kanisa

Kanisa la Kwanza la Wabaptisti nchini Marekani (pia linajulikana kama Jumba la Mikutano la Kwanza la Wabaptisti) ndilo kanisa kongwe zaidi kati ya makanisa ya Wabaptisti nchini Marekani. Kanisa hili lilianzishwa mnamo mwaka 1638 na Roger Williams huko Providence, Rhode Island. Jengo la sasa la kanisa lilijengwa kati ya 1774 na 1775 na lilifanyika mikutano yake ya kwanza mnamo Mei 1775. Kanisa hili liko katika 75 North Main Street kwenye kitongoji cha College Hill huko Providence. Lilitangazwa kuwa Kivutio cha Kitaifa cha Kihistoria mnamo 1960. Kanisa hili lina uhusiano na Makanisa ya Wabaptisti wa Marekani (ABCUSA).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Roger Williams alikuwa akifanya ibada za kidini nyumbani kwake kwa karibu mwaka mmoja kabla ya kugeuza mkutano wake kuwa kanisa la Wabaptisti mnamo 1638. Hii ilifuatia kuanzishwa kwa mji wa Providence mnamo 1636. Kwa mu'da wa miaka sitini iliyofuata, waumini walikutana katika nyumba za waumini wenzao au nje wakati wa hali nzuri ya hewa. Wabaptisti wa Rhode Island katika karne ya 17 waliepuka kujenga majumba ya mikutano kwani walihisi kuwa majengo hayo yalionyesha majivuno. Hata hivyo, baadaye walitambua umuhimu wa kuwa na sehemu ya kukusanyika, na hivyo wakajenga majumba ya mikutano kwa mtindo wa kawaida, sawa na yale ya Wakakeri.

Roger Williams alikuwa Mkalvini, lakini ndani ya miaka michache tangu kuanzishwa kwake, waumini waligeukia zaidi Arminianismu, na kufikia 1652 kanisa lilikuwa wazi kuwa la General Six-Principle Baptist. Lilisalia kuwa kanisa la General Baptist hadi liliporejea katika aina fulani ya Kalvinismu chini ya uongozi wa James Manning katika miaka ya 1770. Aliyefuata baada ya Williams kama mchungaji wa kanisa hili alikuwa Chad Brown, mwanzilishi wa familia mashuhuri ya Brown ya Rhode Island. Barabara kadhaa za Providence zinaitwa kwa majina ya wachungaji wa Kanisa la Kwanza la Wabaptisti, zikiwemo Williams, Brown, Gregory Dexter, Thomas Olney, William Wickenden, Manning, na Stephen Gano.

Mnamo 1700, Pardon Tillinghast alijenga jengo la kwanza la kanisa, lenye ukubwa wa takriban futimraba 400 na mita 37, karibu na kona ya Smith na North Main Streets. Mnamo 1711 alilitoa jengo hilo na ardhi kwa kanisa katika hati iliyoeleza kuwa kanisa hilo lilifuata mafundisho ya General Six-Principle Baptist. Mnamo 1736, waumini walijenga jumba lao la pili la mikutano katika kiwanja kilicho karibu na kona ya Smith na North Main Streets, lenye ukubwa wa takriban futimraba 600.

Uhusiano na Chuo Kikuu cha Brown

[hariri | hariri chanzo]

Moja ya harakati kuu za kutafuta kutambulika zaidi kwa Wabaptisti ilikuwa kuanzishwa kwa taasisi ya elimu kwa ajili ya uchungaji na kuanzishwa kwa chuo kikuu. Jumuiya ya Makanisa ya Wabaptisti ya Philadelphia ilimtuma James Manning Rhode Island kuanzisha chuo kikuu katika koloni la Rhode Island na Providence Plantations mnamo 1764 (ambacho baadaye kilibadilishwa jina kuwa Chuo Kikuu cha Brown). Baada ya kuanza huko Warren, chuo kilihamishiwa Providence mnamo 1770. Rais wa chuo, Manning, pia alichaguliwa kuwa mchungaji wa kanisa la Providence mnamo 1771. Wakati wa uongozi wake, Jumba la Mikutano la sasa lilijengwa "kwa ajili ya ibada ya hadharani ya Mungu Mwenyezi na pia kwa ajili ya sherehe za mahafali.

Ujenzi, marekebisho na hadhi ya kihistoria

[hariri | hariri chanzo]

Ujenzi wa jengo la sasa ulianza majira ya joto ya 1774 na ulikuwa mradi mkubwa zaidi wa ujenzi kuwahi kufanywa New England.[1] Baada ya bandari za Massachusetts kufungwa na Waingereza kama adhabu kwa Boston Tea Party, wajenzi wa meli waliokosa kazi na seremala walikuja Providence kufanya kazi kwenye jengo hilo. Sehemu kuu ya jengo hili ilizinduliwa katikati ya Mei 1775, na mnara wake ulijengwa kwa siku tatu na nusu katika wiki ya kwanza ya Juni. [2]

Jengo hili lilitambuliwa kama Kivutio cha Kitaifa cha Kihistoria mnamo 1960 na likasajiliwa katika Orodha ya Kitaifa ya Maeneo ya Kihistoria mnamo 1966.

Mbali na ibada za kila wiki, Jumba la Mikutano linatumika kwa matamasha, hotuba, na mihadhara ya wasanii, wanazuoni, na viongozi wa kisiasa mashuhuri duniani. Chuo Kikuu cha Brown kinafanya sherehe zake za kuhitimu hapa tangu 1776. [3]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-22. Iliwekwa mnamo 2025-03-30.
  2. https://books.google.com/books?id=fgc2AAAAIAAJ
  3. https://www.brown.edu/Administration/News_Bureau/2004-05/04-124.html
  4. "Images of Brown". library.brown.edu. Iliwekwa mnamo 2020-10-17.