Kanisa kuu la Santiago de Compostela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa kuu kwa nje.

Kanisa kuu la Santiago de Compostela ni kanisa mashuhuri lililoko Santiago de Compostela, huko Galicia nchini Hispania. Umaarufu wake umetokana kwanza na imani kwamba hapa lina kaburi la Mtakatifu Yakobo Mkubwa aliyekuwa labda mdogo wa Yesu na mmoja wa mitume wake.

Jina la Kihispania "Santiago" ni kifupi cha "Mtakatifu Yakobo" (Tiago = Yakobo).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mahali palianza kutambuliwa kama kaburi la mtume huyo mnamo mwaka 814. Mwaka 829 kanisa la kwanza lilijengwa hUKO[1].

Mnamo mwaka 997 kanisa hilo liliharibiwa katika mashambulio ya jeshi la Waarabu na baada ya hao kufukuzwa katika sehemu hiyo ya Hispania, kanisa lilijengwa upya miaka ya 1075 hadi 1211[2].

Jengo hilo liliendelea kuwa shabaha ya wahiji Wakristo kutoka pande zote za Ulaya.

Kanisa lilipanuliwa na kupambwa kwenye karne za 16, 17 na 18.

Jengo ni muundo wa Mtindo wa Kiroma na nyongeza za Mtindo wa Kigothi na wa Baroko baadaye.

Kanisa limepokewa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]