Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam
Mandhari
Kanisa kuu la Mtakatifu Joseph (kwa Kiingereza: St Joseph Cathedral church) ni kanisa lililopo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, mkabala na Sokoine Drive, likiangalia Waterfront, karibu na geti la boti zinazoelekea Zanzibar.
Kanisa hili lilijengwa kwa umahiri na wamisionari Wabenedikto kuanzia mwaka 1897 hadi 1902[1] likatabarukiwa mwaka 1905.[2]. Hadi sasa ni kanisa kuu la Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Mtindo uliofuatwa ni mtindo wa Kigothi mamboleo. Kati ya sifa zake, mojawapo ni vioo vya rangi nyuma ya altare[3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Michael Hodd, East Africa Handbook: The Travel Guide, p. 344
- ↑ (Kiitalia) St. Benedict Monastery Archived 2012-08-02 at Archive.today
- ↑ St. Joseph's Cathedral at Lonely Planet
6°49′10″S 39°17′17″E / 6.81944°S 39.28806°E
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |