Nenda kwa yaliyomo

Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abasia ya Mt. Maria huko Grottaferrata, Roma, Italia, haiko chini ya askofu yeyote.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Linafuata mapokeo ya Ukristo wa Ugiriki na kutumia liturujia ya Ugiriki.

Tangu mwanzo wa Kanisa katika rasi ya Italia kulikuwa na Wakristo waliotumia lugha ya Kigiriki, hata mjini Roma, lakini hasa katika maeneo ya kusini.

Baada ya kutokea Ukristo wa mashariki na Ukristo wa magharibi, maeneo hayo yalishindaniwa.

Wakristo wa mashariki nchini Italia waliongezeka hasa baada ya Albania kuvamiwa na Waturuki Waislamu. Hapo Waalbania wengi walivuka bahari na kukimbilia usalama hasa katika Ufalme wa Sicilia.

Ingawa wengi walimezwa na mazingira mapya, wengine walidumisha lugha yao ya Kialbania pamoja na madhehebu ya Kigiriki.

Hatimaye walipewa na Papa uongozi kamili (6 Februari 1784) na hatimaye (1919) walianzishiwa majimbo mawili, mbali na monasteri huru ya Grottaferrata.

Mwaka 2010, waamini wa Kanisa hilo walikadiriwa kuwa 61,000 hivi katika parokia 45, chini ya maaskofu 2, mapadri 82 (baadhi wakiwa na ndoa) na mashemasi 5. Pia kulikuwa na watawa wasio na daraja takatifu 207.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Ronald Roberson. "The Eastern Catholic Churches 2010" (PDF). Catholic Near East Welfare Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-09-23. Iliwekwa mnamo December 2010. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help) Information sourced from Annuario Pontificio 2010 edition

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Kibizanti nchini Italia kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.