Kamshange
| Mariam Shwaibu Juma | |
| Amezaliwa | Mei 15, 1994 Moshi, Kilimanjaro, Tanzania |
|---|---|
| Nchi | Mtanzania |
| Majina mengine | Kamshange Kahusika |
| Kazi yake | Mtangazaji, muigizaji, mbunifu wa mavazi |
Mariam Shwaibu Juma (alizaliwa 15 Mei 1994) ni mtangazaji wa runinga na redio, muigizaji, na mbunifu wa mavazi na mwanamitindo kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi jina la Kamshange hasa kupitia kipindi chake cha 'Mgundini' kinachorushwa kupitia Clouds TV.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Mariam alizaliwa katika Hospitali ya Mawenzi, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Alisoma shule ya msingi katika Mkuranga Primary School (Pwani), na baadaye akaendelea na elimu ya sekondari katika Msaranga Secondary School huko Moshi.
Aliendelea na masomo ya uandishi wa habari katika chuo cha kati cha DSJ (Dar es Salaam School of Journalism). Akiwa mwaka wa pili chuoni, alishiriki mashindano ya urembo ya chuo hicho na kutwaa taji la 'Miss DSJ' mwaka 2013. Mwaka uliofuata, alishiriki katika mashindano ya Miss Open University of Tanzania (OUT) na kuwa mshindi wa kwanza, na hatimaye kuiwakilisha OUT kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2014.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2020, Mariam alipata nafasi ya kujiunga na Clouds Media Group kama mtayarishaji wa kipindi cha redio cha Amplifaya. Baadaye, alipata fursa ya kuandaa na kuendesha kipindi chake cha runinga kiitwacho 'Mgundini', kinachorushwa kila Jumamosi saa 10:30 jioni kupitia Clouds TV.
Uigizaji
[hariri | hariri chanzo]Mbali na kazi ya utangazaji, Mariam ni mwigizaji aliyeshiriki katika filamu mbalimbali za Kitanzania, zikiwemo Nazi Bubu na Mawio.