Nenda kwa yaliyomo

Kampuni ya DVS

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kampuni ya viatu ya DVS
Jina la kampuni Kampuni ya viatu ya DVS
Ilianzishwa 1995
Mwanzilishi Kevin Dunlap
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji na Uuzaji
Makao Makuu ya kampuni Torrance,California
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii * Viatu
* Vifaa vya spoti mbalimbali
Nchi Marekani
Tovuti http://www.dvsshoes.com/

Kampuni ya viatu ya DVS ilianzishwa katika mwaka wa 1995 na Kevin Dunlap akiwa pamoja na Tim Gavin.

DVS huwa na makao yao Torrance, California na inamilikiwa na kampuni ya usambazaji ya Podium Distribution.Neno la ufupisho 'DVS' linasemekana kusimamia "Devious" likimaanisha kwa Swahili 'mjanja'.

DVS ,hapo awali, iliunda viatu maalum vya wanaume vya skateboard lakini ,hivi leo, imepanua aina zao za viatu kuhusu ,pia, vya wanawake ,vya vijana na vya watoto wadogo. Viatu hivi si vya skateboard pekee bali ni vya aina mbalimbali kama vile vya mitindo mbalimbali ya starehe. Wameanzisha pia kushona nguo za kuuzwa.

Katika mwaka wa 2007, walianza aina ndogo ya viatu iliyoitwa Luxe,ambayo ilihusisha mitindo mipya na kutengenezwa kwa matumizi ya vifaa vilivyokuwa ghali kidogo.Usambazaji wa viatu vya aina hii ulikuwa mdogo na havikuwa vinaenezwa katika eneo kubwa.

Timu yao imepanua shughuli zake mbalimbali hadi inatoa udhamini kwa wanamichezo wa mchezo wa kutumia bodi ya aina ya skateboard hadi wanamichezo wa kuendesha pikipiki na michezo mingine mbalimbali.

Wanachama maarufu wa timu hii inahusisha Zered Bassett, Steve Berra, Kerry Getz, Daewon Song, na Jeron Wilson.

Viatu na Bidhaa ya DVS[hariri | hariri chanzo]

DVS inaathiriwa na hulka na mitindo ya wanachama maarufu wa timu yake ya wanamichezo (wanamichezo wa skateboard ,pikipiki na wa michezo mingine).Hivyo basi,inahusisha aina mbalimbali za bidhaa huku ikiendeleza umakini katika utengenezaji wa bidhaa wakitilia maanani mahitaji ya wanamichezo wa kutumia bodi ya skateboard duniani kote.

"Wamehusika katika skateboard" tangu mwaka wa 1995.

Timu ya ina waendeshaji bora kabisa katika michezo ya uendeshaji wa pikipiki wa siku hizi kama vile: Daewon Song,Kerry Getz, Steve Berra na Torey Pudwill. Kwa kutumia wanachama wa timu yao, DVS huweka viatu vyao na bidhaa zao katika majaribio ngumu kabisa kabla ya kuanza kuzitengeneza kwa kuuza kwa umma.Teknolojia inayotumika na DVS ni kama:

  • Bruise Control™ ya kulinda mguu kutoka madhara na majeraha,
  • ECOTRUE™- ambayo inahusisha kutumiwa kwa vifaa vinavyoweza kutumika 100% tena katika utengenezaji wa viatu na
  • CGT™ ambayo inasaidia madereva waweze kuendelea kushikilia usukani vizuri hata katika misimu ya baridi kali.

DVS inatengeneza ,pia, viatu , nguo na bidhaa mbalimbali zinazotumika katika michezo zozote za kutumia bodi.

DVS inaendelea kuuza bidhaa zake kwa soko na kuboresha vipengele vyote vya bidhaa zao zinazotumika katika michezo ya bodi kama mchezo wa skateboard,mchezo wa kuteleza na bodi kwenye theluji na mchezo wa kubobea kwenye maji ukitumia bodi. Kampuni hii imenawiri sana katika sekta hii na itaendelea kushinikiza maendeleo katika spoti hizo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Aina za viatu ya DVS