Nenda kwa yaliyomo

Kagendo Murungi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kagendo Murungi
AmezaliwaKagendo Murungi
(1971-12-07)7 Desemba 1971
Amekufa27 Desemba 2017 (umri 46)
Harlem, New York, U.S.
UtaifaKenya

Kagendo Murungi (7 Desemba 197127 Desemba 2017) alikuwa Mkenya mpigania haki za wanawake, haki za LGBT na mtengenezaji wa filamu. Alifanya kazi kama wakili na mtetezi wa haki za jamii ya LGBTQ ya Afrika kwa zaidi ya miongo miwili.

Kagendo Murungi alizaliwa nchini Kenya na alikuwa na ndugu sita.[1] Alihamia Marekani ambako aliishi kwa muda mrefu wa maisha yake.

Kagendo alipata shahada yake katika masomo ya wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Rutgers na kuendelea na shahada ya uzamili katika masomo ya vyombo vya habari kutoka Shule Mpya ya Utafiti wa Jamii. Aliendelea na kazi yake katika tasnia ya filamu kama mkurugenzi na mtayarishaji wa filamu. Alianzisha studio ya utengenezaji wa filamu ya Wapinduzi Productions mnamo 1991 na alihudumu kama mtayarishaji mkuu wake kwa takriban miaka 26.[2] Alisimulia hadithi ya filamu ya hali halisi ya Marekani ya 1995 These Girls Are Missing.

Alihusika katika kuunda nafasi ya afisa programu wa Afrika katika Tume ya Kimataifa ya Haki za Kibinadamu ya Mashoga na Wasagaji. Pia alihudumu kama msaidizi wa hiari kwa Tamasha la Filamu la Kiafrika kwa miaka 15.[3] Pia alishikilia wadhifa wa Mshiriki wa Programu na Muungano wa Kitaifa wa Uratibu wa Vipindi vya Televishenivya Weusi alipokuwa angali mratibu wa jamii. Mnamo 2016, alihudumu kama mkurugenzi wa Hazina ya Chakula katika Kanisa la St. Mary's, Harlem.

Mnamo Agosti 2021, Shirika la kimataifa la Utetezi, Global Citizen, lilimtambua kama miongoni mwa wanawake wana harakati saba wa Kiafrika wanaostahili kutengewa makala katika Wikipedia.[4]

Aliaga dunia tarehe 27 Desemba 2017 akiwa na umri wa miaka 46 katika makazi yake Huko Harlem. Alizikwa Katika shamba la familia lao nchini Kenya.[5]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. obituary (2018-01-18). "Kagendo Murungi". Obituary Kenya (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-10. Iliwekwa mnamo 2021-08-10.
  2. "Murungi, Kagendo | African Film Festival, Inc" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-08-10.
  3. "Murungi, Kagendo | African Film Festival, Inc" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-08-10."Murungi, Kagendo | African Film Festival, Inc". Retrieved 2021-08-10.
  4. "7 Notable African Women Activists Who Deserve Wikipedia Pages". Global Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-10.
  5. mmoneymaker (2018-01-02). "Remembering Activist Kagendo Murungi". OutRight Action International (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-10.