Kabalega wa Bunyoro

Chwa II Kabalega (18 Juni 1853 – 6 Aprili 1923) alikuwa mfalme au Omukama wa Bunyoro huko Uganda miaka 1870 - 1899.
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 1869, Omukama Kamurasi Kyebambe IV alifariki dunia na wagombea halali wa kifalme- Kabalega na kabigumire hawakuweza kukubaliana ni nani angechukua urithi wake. Hii ilisababisha vita vya kurithi vikali katika Dola ya Kutara.[1] Kawaida vita kama hivi vya kuamua mrithi halali vilitarajiwa kuwa vifupi na vya uamuzi haraka hadi mmoja tu kati ya wagombea wa kiti cha enzi abaki hai.[2] Hata hivyo wakati mwingine migogoro hii ingeendelea kwa miaka, ikileta kutokuwepo kwa utulivu katika jamii nzima na kusababisha njaa, mauaji na migogoro ya wakimbizi. Katika kesi hii viongozi wa ukoo na kaka wa mfalme aliyefariki, Prince Nyaika, walikuwa wamechoka kutokana na vita vya mara kwa mara kati ya Kabalega na Kabigumire kiasi kwamba waliamuru Kabalega ambaye alikuwa na nguvu zaidi , kuheshimu sheria za kurithi Bunyoro na kanuni za vita halalina kumaliza vita. Wakati Kabalega alipochaguliwa kuwa mfalme, aliwazia kuendeleza dola yake mpya kupitia biashar, hasa kupitia Kibiro Saltworks. Mnamo 1 Januari 1894,Waingereza walitangaza vita dhidi ya Bunyoro. Wakati wa kilele cha shambulio la Waingereza dhidi ya dola yake, Kabalega alikimbia na kujificha katika Acholi chini ya ulinzi wa kiongozi Awich Abok wa Payira. Kutoka hapo aliendela kuongoza Kikosi cha mapinduzi cha Nyangire ambacho kilithibitisha kuwa kichungu kwa wakoloni Waingereza
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Chisholm, Hugh, (22 Feb. 1866–29 Sept. 1924), Editor of the Encyclopædia Britannica (10th, 11th and 12th editions)", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2025-10-15
- ↑ "Order in council by His/Her Majesty's most honourable Privy Council, Wednesday, 8 July 1761 [fauqfrVH0020547a1d]". Electronic Enlightenment Scholarly Edition of Correspondence. 2025-03. Iliwekwa mnamo 2025-10-15.
{{cite web}}: Check date values in:|date=(help)
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kabalega wa Bunyoro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |