Just Fontaine

Just Louis Fontaine (hutamkwa ; 18 Agosti 1933 – 28 Februari 2023) alikuwa mchezaji wa soka la kulipwa kutoka Ufaransa aliyecheza katika nafasi ya mshambuliaji.
Fontaine ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika Kombe moja la Dunia la FIFA, baada ya kufunga mabao 13 katika mechi 6 katika Kombe la Dunia la 1958.
Mwezi Machi 2004, Pelé alimtaja Fontaine miongoni mwa wachezaji 125 bora zaidi waliokuwa hai duniani, katika hafla ya tuzo za FIFA.
Maisha ya Awali na Maisha ya Soka
[hariri | hariri chanzo]Fontaine alizaliwa Marrakesh, Morocco, akiwa mtoto wa baba Mfaransa na mama mwenye asili ya Hispania. Baadaye alihamia Casablanca, ambako alisoma katika Lycée Lyautey.
Fontaine alianza kucheza soka kwa kiwango cha amateur katika klabu ya US Marocaine, ambako alicheza kuanzia 1950 hadi 1953.
Mwaka 1953, klabu ya Nice ilimsajili. Akiwa Nice, alifunga mabao 44 katika misimu mitatu. [1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.fff.fr/equipe-nationale/joueur/9771-fontaine-just/fiche.html[dead link]
- ↑ https://web.archive.org/web/20150905220314/http://www.fifa.com/fifa-tournaments/players-coaches/people=29875/index.html
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Just Fontaine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |