Juma Mwapachu
Juma Volter Mwapachu (27 Septemba 1942 – 28 Machi 2025) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania ambaye alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.[1] Alichukua nafasi ya Amanya Mushega wa Uganda ambaye alimaliza muhula wake wa miaka mitano mnamo 24 Machi 2006. Aliteuliwa kwa wadhifa huo na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC tarehe 4 Aprili, 2006. Kabla ya uteuzi huu, Mwapachu alikuwa Balozi wa Heshima na Plenipotentiary na mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika UNESCO.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mwapachu alihitimu sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (shahada aliyoipata mwaka 1969.) Pia alikuwa na Stashahada ya Uzamili katika Sheria za Kimataifa, Taasisi za Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Sheria za Kimataifa na Diplomasia cha India, New Delhi, India. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilimtunuku Shahada ya Udaktari wa Fasihi (Heshima - *Honoris Causa*) mwaka 2005. Alifariki tarehe 28 Machi, 2025 akiwa na umri wa miaka 82.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "AU head urges Kenya peace deal", BBC News, BBC, 22 Februari 2008, iliwekwa mnamo 3 Mei 2010
{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Juma Mwapachu Takes Over as Secretary General
| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Juma Mwapachu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |