Juma Hamad Omar
Mandhari
Juma Hamad Omar ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CUF. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Ole kwa miaka 2015 – 2020. [1]
Juma Omar alipata elimu yake ya msingi Skuli ya msingi Ngambwa (1960-1968) baadae kujiunga na elimu ya sekondari Fidel Castro (1969-1972) baadae elimu ya sekondari ya juu Lumumba (1973-1974).
Juma Omar alipata shahada yake ya mwanzo ya ualimu akibobea katika somo la fizikia chuo kikuu cha Dar es Salaam (1975-1978) na baadae kujiunga na chuo kikuu cha Reading (1980-1981) na kuchukua shahada ya uzamivu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania Ilihifadhiwa 25 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., iliangaliwa Mei 2017
| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Juma Hamad Omar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |