Julie-Victoire Daubié
Julie-Victoire Daubié (26 Machi 1824 – 26 Agosti 1874) alikuwa mwanahabari wa Ufaransa. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuhitimu katika chuo kikuu nchini Ufaransa alipopata shahada ya leseni (licence) huko Lyon mwaka 1871.
Baadhi ya kazi zake zilitafsiriwa kwa Kiingereza na Josephine Butler.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Daubié alizaliwa tarehe 26 Machi 1824 katika mji wa Bains-les-Bains, katika eneo la Vosges. Baba yake alifariki akiwa bado na umri wa chini ya miaka miwili, na yeye pamoja na ndugu zake saba walihamia Fontenoy pamoja na mama yao kuishi na familia ya upande wa baba.
Alisoma Kilatini, Kigiriki, Kijerumani, historia na jiografia kwa msaada wa kaka yake. Mwaka 1844 alipata cheti cha ualimu na baadaye alisomea zoolojia katika Makumbusho ya Historia ya Asili huko Paris, ambako alifundishwa na mtaalamu mashuhuri Geoffroy Saint-Hilaire.
Licha ya kuwa na elimu nzuri na kutokuwepo kwa sheria zilizowazuia wanawake kujiunga na vyuo vikuu, Daubié alikataliwa mara kadhaa kujiunga na vyuo mbalimbali nchini Ufaransa. Hata hivyo aliendelea kuhudhuria masomo huku akifanya kazi kama mlezi (governess).
Elimu na kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1859, Daubié alishiriki shindano la insha lililoandaliwa na Chuo cha Kifalme cha Sayansi na Fasihi cha Lyon. Aliandika kazi yenye karibu kurasa 300 yenye kichwa Mwanamke Maskini katika Karne ya 19: Hali na Fursa za Wanawake, iliyochambua ubaguzi wa kitaaluma na kielimu dhidi ya wanawake, tofauti za mishahara, na changamoto nyingine. Insha hiyo ilishinda tuzo ya kwanza na kumfungulia njia ya kukubaliwa.
Mwaka 1861, alikua mwanamke wa kwanza kujitokeza kufanya mtihani wa baccalauréat nchini Ufaransa. Alikuwa na umri wa miaka 37 alipofaulu na kuwa mwanamke wa kwanza kupata cheti hicho nchini humo.
Baada ya kuhitimu, aliendelea kuandika kuhusu hali ya wanawake kama mwanaharakati na msomi. Alinunua nyumba kubwa huko Fontenoy ambako alianzisha biashara ya ushonaji wa mapambo (embroidery) aliyomkabidhi mpwa wake.
Pia aliishi katika barabara ya Champs-Élysées huko Paris na kuwa mwanahabari wa masuala ya uchumi aliyefahamika. Mwaka 1871 alipata shahada ya sanaa (arts) huko Lyon, na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kupata shahada ya leseni katika fasihi. Aliendelea kuwa mtetezi wa haki za wanawake na pia mwanahabari
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Daubié alifariki tarehe 25 Agosti 1874 akiwa na umri wa miaka 50 huko Fontenoy-le-Château, katika eneo la Lorraine, kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu (tuberculosis).
Urithi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Machi 2018, aliheshimiwa na Google kupitia mchoro maalum wa "Google Doodle".
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julie-Victoire Daubié kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |