Nenda kwa yaliyomo

Juliani wa Cuenca

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Juliani alivyochorwa na Eugenio Cajes.

Juliani wa Cuenca (Burgos, Castilia Mpya, Hispania, 1127 hivi - Cuenca, Aragon, Hispania, 28 Januari 1208) alikuwa mkaapweke[1], lakini pia mhubiri na mwalimu, aliyehudumia kama askofu wa Cuenca kuanzia mwaka 1196 hadi kifo chake[2].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu hasa baada ya kutangazwa rasmi na Papa Klementi VIII tarehe 18 Oktoba 1594.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Januari[3].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kukabidhiwa jimbo, lililokombolewa tangu miaka michache kutoka mikononi mwa Waislamu, alijitahidi kutembelea parokia zake na kuhudumia wafungwa bila kuacha kurudi upwekeni kila mwaka.

Kwa kuwa alikuwa amewagawia maskini mali ya Kanisa, alijipatia riziki kwa kazi ya mikono yake[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Julian of Cuenca, St.. New Catholic Encyclopedia (2003). Retrieved on 11 October 2017.
  2. Saint Julian of Cuenca. Saints SQPN (25 January 2017). Retrieved on 11 October 2017.
  3. Martyrologium Romanum
  4. Book of the Saints, Kessinger Publishing, 2003, page 156

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.