Nenda kwa yaliyomo

Juliana Rotich

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Juliana Rotich (alizaliwa 1977) ni mtaalamu wa teknolojia ya habari kutoka nchini Kenya, ambaye ametengeneza zana za mtandaoni kwa ajili ya kukusanya taarifa za majanga kutoka katika jamii (crowdsourcing) na kuripoti mada zinazohusiana na mazingira.

Ni mwasisi mwenza wa iHub, kituo cha pamoja cha teknolojia jijini Nairobi, Kenya, na Ushahidi, programu huria ya kukusanya na kuainisha taarifa kwenye ramani. Pia, ni mwanachama mwandamizi wa TED (TED Senior Fellow).[1]

Ni mdhamini wa Wakfu wa Bankinter kwa ajili ya Ujasiriamali na Ubunifu nchini Uhispania, pamoja na mjumbe wa Bodi ya Utekelezaji ya Kenya Vision 2030. Alikuwa mkuu wa kanda ya nchi za Afrika Mashariki kwa kampuni ya BASF kuanzia Mei hadi Desemba 2018.[2]

Historia na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Rotich baada ya kusoma elimu ya msingi na sekondari nchini kwao, alipokelewa katika Chuo Kikuu cha Missouri–Kansas City nchini Marekani. Alihitimu kutoka chuoni hapo akiwa na shahada ya Sayansi (Bachelor of Science) katika Sayansi ya Kompyuta. Pia ni Mshiriki wa MIT Media Lab (MIT Media Lab Fellow).[2]

  1. TED Conference (Juni 2013). "Juliana Rotich Technology Entrepreneur". New York City: TED Conference. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 1 2 BASF (23 Mei 2018). "BASF Appoints Kenyan Juliana Rotich as Country Cluster Head for East Africa". Ludwigshafen, Germany: BASF. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2019. Iliwekwa mnamo 2 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juliana Rotich kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.