Nenda kwa yaliyomo

Judith Herzberg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Judith Frieda Lina Herzberg (alizaliwa 4 Novemba 1934) ni mshairi na mwandishi kutoka nchi ya Uholanzi.

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Judith Herzberg ni binti wa mwanasheria na mwandishi Abel Herzberg.[1] Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Herzberg aliishi kwa kujificha katika maeneo mbalimbali. Tangu mwaka 1983, Herzberg amekuwa akiishi kwa kupishana kati ya nchi ya Uholanzi na Israel.[1] Anaandika zaidi mashairi na michezo ya kuigiza, na pia anajihusisha na uandaaji wa filamu. Herzberg alifanya mwanzo wake (debut) kama mshairi mnamo mwaka 1961 katika gazeti la kila wiki la Vrij Nederland. Miaka miwili baadaye, alichapisha mkusanyiko wake wa kwanza wa mashairi ulioitwa Zeepost. Pia aliandika michezo ya kuigiza ya Leedvermaak, Charlotte, na Rijgdraad, ambayo iligeuzwa kuwa filamu na Frans Weisz. Michezo ya Charlotte inamuhusu mchoraji Charlotte Salomon aliyeuawa katika Kambi ya mateso ya Auschwitz.[2] Mnamo mwaka 1997, Herzberg alipokea Tuzo ya P. C. Hooft (P. C. Hooft Award) kwa ajili ya mchango wa kazi zake zote. Katika mwaka wa 2018, alitunukiwa tuzo ya Prijs Der Nederlandse Letteren (Prijs der Nederlandse Letteren).[3]

  1. 1 2 "Schrijvers en dichters (dbnl biografieënproject I)". Digital Library for Dutch Literature (kwa Kiholanzi). 2013. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "De Nederlandse en Vlaamse auteurs". Digital Library for Dutch Literature (kwa Kiholanzi). 1985. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. https://taalunie.org/actueel/27/judith-herzberg-krijgt-prijs-der-nederlandse-letteren-2018
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Judith Herzberg kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.